Featured Post

SIKU YA PILI YA SAFARI YA WANAHABARI NA ASKARI WA JESHI LA ULINZI ,KUELEKEA KILELE CH UHURU ,MLIMA KILIMANJARO.

Baada ya mapumzko ya siku ya kwanza katika kituo cha Mandara,timu ya Wanahabari na Asakari wa jeshi la Ulinzi asubuhi yake walipanga mstari mmoja kwa ajili ya kuanza safari ya kuelekea kituo cha pili cha Horombo.
Safari ilianza  kwa kila mshiriki kuoenkana mwenye afya na nguvu ya kufikia ndoto ya kufika kilele cha Uhuru.
Baada ya kupita katika msitu mnene wakati wa kuanza safari uelekeo wa kituo cha Mandara na baadae kutoka Mandara kuelekea Horombo,kidogo kidogo hali ya uoto ilionekana kubadilika kadri washiriki walivyokuwa wakielekea sehemu za juu.
Mwendo wa takribani saa saba kuanzia majira ya saa 2:30 asubuhi  kutokea Mandara.Washiriki wakafika eneo la nusu njia kuelekea Horombo na kupata chakula cha Mchana.
Safari ikaendelea.
Hatimaye majira ya saa 11 jioni ,timu ya Wanahabari na Askari wa jeshi la Ulinzi wakaingia katika kituo cha Horombo.
Kama ilivy ada kuchukua kumbukumbu likawa jambo la muhimu kwao ,na hapa wakapa picha ya pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu na Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi TANAPA,Jenerali George Waitara  aliyekuwa mkuu wa msafara.
Majira ya usiku wa saa moja ,timu ilipata chakula cha usiku na maelekezo kutoka kwa mkuu wa waongoza watalii ,Chombo kwa ajili ya siku iliyofuata.
Siku iliyofuata ilikua ni siku ya mazoezi ,siku hii ilitengwa kwa ajili ya kuzoea hali ya hewa ya juu wenyewe wanaita "Climatization",mazoezi yalikuwa ni kufanya safari ya kueleke eneo lijulikanalo kama Zebra.
Safari ya kuelekea Zebra ikaanza.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu ,Jenerali George Waitara pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii ,Mstaafu ,Balozi Charles Sanga pia walikuwa katika safari hiyo ya mazoezi.
Hatimaye timu ikafika eneo la Zebra.
Baadahi yao Washiriki wakapata nafasi ya kupata kumbukumbu na wageni kutoka Japan walikuwa wakipanda mlima Kilimanjaro kama Watalii.
Timu ikapata picha ya pamoja na Naibu Kamanda wa kikosi cha Ardhini,Brigedia Jenerali ,Jairo Mwaseba baada ya kufika katika eneo la Zebra.
Eneo la Zebra umaarufu wake unatokana na michoro iliyopo katika Mawe makubwa ikiwa mithili ya pundamilia.
Majira ya jioni baada ya kurudi kituo cha Mandari, timu ilijiandaa na safari ya kuekeea kituo cha Kibo, hali ya hewa eneo hili ilikuwa ni ya kubadilika badilika kila mara zaidi baridi ikiambatana na ukungu ndio ilitawala.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii aliyekuwa katika safari hiyo.

Comments