Featured Post

MAJANGA MAKUBWA! MCHELE WA PLASTIKI WAZAGAA MITAANI... SHUHUDIA VIDEO JINSI WACHINA WANAVYOUTENGENEZA!


Na Daniel Mbega
LICHA ya serikali kuwaondoa hofu Watanzania kuhusu kuzagaa kwa mchele unatengenezwa kwa plastiki (synthetic rice) kutoka China kwamba haupo, mchele huo bado unadaiwa upo mitaani katika maduka mbalimbali, imefahamika.

Taarifa zinasema kwamba, mchele huo umekuwa ukiingia nchini kwa magendo kama ilivyo kwa biashara nyingine haramu zikiwemo dawa za kulevya, na kwamba biashara ya kusambaza mchele huo wa plastiki inafanywa na wafanyabiashara wakubwa nchini wakishirikiana na maswahiba zao kwenye mtandao kutoka China kama ilivyo mitandao mingine ya kihalifu.
Desemba 15, 2016, serikali kupitia Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), ilikanusha kuwapo kwa viwanda vya Kichina vinavyotengeneza mchele huo nchini na kuwataka wananchi wapuuze taarifa hizo.
Meneja Mawasiliano na Mahusiano kwa Umma kutoka TFDA, Gaudensia Simwanza alisema hakuna ukweli wowote juu ya taarifa hizo bali ni uzushi wa watu waliokosa kazi na wanaotaka kuwachanganya na kuwatia hofu Watanzania.
“Kwanza naomba niulize hivi mchele wa plastiki ukiupika unaiva? Je, kuna mtu yeyote aliyewahi kuununua mchele wa aina hiyo? Kama yupo tunaomba ajitokeze aseme na atupe ushahidi wa kujitosheleza,” alisema Bi. Simwanza.
Inaelezwa kwamba, mchele wa plastiki unaiva ukipikwa, lakini unanata na una harufu ya kemikali kwa mbali.
Lakini wakati Tanzania inakanusha kuwepo kwa mchele huo licha ya historian a uzoefu kuonyesha kwamba nchi hiyo imekuwa jalala la bidhaa feki na rahisi kuingizwa nchini, tayari nchini Kenya wananchi wameanza kupiga kelele kwamba mchele huo wa plastiki umekwishavamia soko.
Desemba 28, 2016, wakulima wa mpunga wa eneo la Kirinyaga, katika Jimbo la Central nchini Kenya waliitaka serikali kuchukua hatua za haraka kwa maelezo kwamba mchele wa plastiki umekwishavamia soko na unaingizwa kwa njia za magendo kutoka China.
Mkurugenzi wa Bodi ya Huduma za Maji ya Tana Athi, Mureithi Kang’ara, alikaririwa akisema kwamba ni jambo la hatari kuona mchele bandia ukiingizwa nchini humo.
Alisema kwamba, baadhi ya watu wanaingiza mchele huo bandia ambao ni wa gharama nafuu na kuufungasha huku wakiwaeleza wateja kwamba ni mchele kutoka Kirinyaga, eneo ambalo ni maarufu kwa kilimo cha mpunga.
Kang’ara alilitaka Shirika la Viwango la Kenya (Kenya Bureau of Standards – KBS) na mamlaka nyingine zinazowajibika kulinda mipaka kusimamia vyema shughuli yao na kuwatia nguvuni wale wambao wanajihusisha na biashara hiyo ambayo siyo tu inaua soko la ndani, lakini pia mchele huo una madhara kwa afya za watumaiji.
Wiki iliyopita, Nigeria ilikamata maguni 100 ya mchele wa plastiki ambao uliingizwa kimagendo nchini humo na kumkamata mtuhumiwa mmoja, huku maofisa wakisema mchele huo haufai kwa matumizi ya binadamu.
Hata hivyo, Desemba 24, 2016, Wizara ya Afya ya Nigeria ilitangaza kwamba mchele huo ‘haukuwa wa plastiki’ ingawa walikiri kwamba haukuwa na nembo za wazalishaji wala nembo ya uthibitisho kutoka Wakala wa Udhibiti wa Chakula na Dawa (National Agency for Food and Drug Administration and Control - NAFDAC).

UKWELI WA MCHELE WA PLASTIKI
China kwa miaka mingi sasa imekuwa ikizalisha mchele wa platiski licha ya nchi hiyo kutajwa kwamba ndiyo kinara wa uzalishaji wa mpunga duniani.
Mchele huo wa plastiki wakati mwingine unatengenezwa kutokana na viazi pamoja na kiasi kidogo cha mchele wa kawaida. Punje za mchele huo feki zinafanana kabisa na mchele wa kawaida lakini huwa ngumu baada ya kupikwa, na taarifa zinasema mchele huo unasafirishwa hadi Marekani.
Mwanahabari mmoja kutoka kituo maarufu cha luninga cha Kiingereza nchini China, Blue Ocean Network, alifichua kwamba mchele wa Wuchang ni feki pia.
Inaelezwa kwamba, katika kila gunia, kiasi kidogo cha mchele halisi huchanganywa na mchele feki, wanapulizia dawa maalum yenye harufu kama ya mchele, kisha kufungashwa na kusambaza sehemu zote za China.
Mwandishi huyo alibaini kwamba, kati ya tani 10 milioni za mchele unaozalishwa Wuchang   kila mwaka, tani milioni 9 ni za mchele feki.
Inaelezwa kwamba, ukila sahani tatu za wali uliotokana na mchele feki ni sawa na kutafuna kiroba kizima, jambo ambalo ni la hatari kwa afya pamoja na mfumo wa mmenyeng’enyo na linaweza kusababisha madhara makubwa yakiwemo vifo vya ghafla.
Tangu mapema mwaka 2011, mitandao ya kijamii ilianza kueleza kwamba mchele wa plastiki ulikuwa unazalishwa nchini China, unasafirishwa nje ya nchi na kutumiwa na watu katika mataifa mengine bila kujua kwamba mchele huo haukuwa chakula kabisa.
‘Mchele’ huo unatengenezwa kwa kuchanganya viazi, viazi vitamu na plastiki. Viazi vinatengenezwa kwanza katika maumbile ya punje za mchele. Baadaye punje hizo zinachanganywa na kemikali maarufu kama synthetic resins. Mchele huo huwa mgumu hata ukipikwa ingawa unanata.
Takriban watu 300,000 waliathirika na watoto sita walikufa mwaka 2008 wakati walipokunywa maziwa feki yaliyotengenezwa kwa fomula maalum na kuchanganywa na kemikali aina  ya melamine.
Ni mwaka huo pia, kemikali ya melamine iligundulika kwenye mayai ya China, ambayo mengi ni feki.
Lakini serikali inaandaa mkakati wa kuhakikisha bidhaa feki kutoka China haziuzwi nchini Tanzania ambapo miezi kadhaa iliyopita ilikamata mitumba ya nguo za ndani tani 6.9, 'ice cream' 1,260, mchele kilo unaodhaniwa kuwa bandia na kuuteketeza.

JINSI YA KUUBAINI MCHELE WA PLASTIKI
 



Nitajaribu kuwaeleza mbinu chache za kuweza kuutambua mchele wa plastiki (kama zinavyoelekezwa kwenye video hiyo hapo juu), mbinu ambazo hazihitaji kemikali bali unaweza kufanya majaribio nyumbani kwako.
Ni vyema sana kuubaini mchele feki, kwa sababu kama hutaweza na ukapikwa na kuliwa na familia, unaweza kusababisha magonjwa yasiyofahamika.
·        Chuku glasi moja ya maji na weka kijiko kimoja cha mchele ndani ya majji hayo. Tikisa kidogo. Utaona kwamba kama mchele huo ni wa plastiki, basi utaelea juu kwa sababu mchele huo ni mchanganyiko wa plastiki ndiyo maana ni rahisi kuelea. Hii ni rahisi sana.
·        Jaribio linguine, chukua mchele na kuuchoma kwa kutumia kibiriti tu. Kama ni mchele wa plastiki basi utasikia harufu ya plastiki baada ya kuuchoma.
·        Unaweza kuujaribu mchele huo baada ya kuupika. Chukua mchele uliochemshwa na kuuweka kwenye chupa moja na uuache kwa siku 2-3. Kama mchele huo ni feki/wa plastiki basi hauwezi kupata kuvu (ukungu) na utakuwa kama ulivyouweka. Kumbuka tu kwamba, plastiki haibadilishwi na hali ya hewa au joto au msimu. Plastiki itabaki vile vile.
·        Jaribio linguine muhimu la kuubaini mchele feki ni kwamba, chukua mchele na utumbukize kwenye maffuta yanayochemka hasa – hata ikiwa katika nyuzijoto 200 C. Utaona kwamba, kama mchele huo ni feki utabaki chini ya sufuria au chungu ama chombo chochote unachopikia. Hauwezi kuja juu na kutokota kama ulivyo mchele wa kawaida.  
·        Utaubaini mchele feki  katika mapishi ya kawaida wakati unachemka tu. Kama ni feki utaona kwamba wote unapanda juu na kuweka utando, tofauti na mchele wa kawaida ambao hubaki chini.




Comments