Featured Post

WASTAAFU WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO KULIPWA MWEZI MMOJA MMOJA

Wastaafu mbalimbali wakiwa kwenye foleni kusubiri zamu yao ya kuhakikiwa jijini Dodoma.

SERIKALI imesema kuwa itaendelea na utaratibu wa kuwalipa wastaafu wanaohudumiwa na Wizara ya Fedha na Mipango, pensheni yao kila mwezi kwa mujibu wa sharia ya mafao ya wastaafu Na. 371 badala ya kuwalipa malipo hayo kila baada ya miezi mitatu.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. DOTTO JAMES amesema kuwa uamuzi huo umetolewa baada ya kupitia na kujadili mapendekezo ya baadhi ya wastaafu waliofika Makao Makao Makuu ya Wizara ya Fedha Jijini Da ers salaam mwezi uliopita wakitaka serikali irejeshe utaratibu wa kuwalipa kila baada ya miezi mitatu mitatu ili waweze kujikimu kimaisha.

James amesema kuwa Wizara imepokea maombi kutoka kwa baadhi ya wastaafu kutaka kulipwa kila baada ya kipindi hicho huku wengine wakitaka kulipwa kila mwezi hatua ambayo imeifanya Serikali kuamua kulifanyia kazi suala hilo kwa kina na kuahidi kulitolea uamuzi hapo baadae.


Benny Mwaipaja, Msemaji Wizara ya Fedha na Mipango

Comments