Featured Post

WAMACHINGA MWANZA WADAI KUTOSHIRIKISHWA KUHAMA



By Juma Ng’oko, Mwananchi
Mwanza. Sakata la wafanyabiashara ndogo (Wamachinga) jijini Mwanza kutakiwa kuhama katikati ya jiji limechukua sura mpya, baada ya kuanza kudai hawajashirikishwa kwenye vikao vya kuwahamisha.

Agosti 11, Rais John Magufuli aliagiza machinga wahamishwe baada ya miezi mitatu badala ya Agosti 20 kama ilivyokuwa imepangwa na uongozi wa mkoa huo.
Hata hivyo, Novemba 23, wakuu wa wilaya za Nyamagana na Ilemela walitoa siku saba hadi Desemba 2, wamachinga wame wamehama kwa hiari.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba (pichani) akizungumza kwa simu amesema kupitia wawakilishi wao, walishiriki vikao na kutembelea maeneo wanayotakiwa kuhamia.
“Hata wafanyeje, kazi ya kuwahamisha ipo palepale na watakaokaidi watakumbana na mkono wa sheria,” amesema.
Ameongeza kuwa siyo wote watakaokaidi watapelekwa mahakamani, bali zimeandaliwa adhabu mbadala ikiwamo kufanya usafi ndani ya Mto Mirongo na maeneo mengine ya jiji.
Mwenyekiti wa Shirika la Umoja wa Machinga (Shiuma), Matondo Masanja amekana kuwa uongozi wake haujashirikishwa kwenye vikao vya uamuzi.
CHANZO – MWANANCHI

Comments