Featured Post

WAGANGA WAPELEKWA ‘KUSAIDIA’ KUSAKA DHAHABU



 
By Ernest Magashi, Mwananchi
Bukombe. Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni. Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia uamuzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe mkoani Geita kuingiza waganga wa jadi ndani ya hifadhi yake.

Waganga hao wameingizwa kwa lengo la kufanya tambiko kutokana na wachimbaji kukimbia na kusalia wachache.
Hatua hiyo inadaiwa kusababishwa na dhahabu kupungua, hivyo uamuzi huo utasaidia madini hayo yaongezeke. Baadhi ya wachimbaji waliaza kuitupimia lawama halmashauri kuwa ‘imewaingiza mjini’ kwa kuwatoza Sh100,000 hadi Sh300,000.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Safari Mayala amesema madini hayo haypatikani bila matambiko na kwamba, wameamua kuwashirikisha waganga hao maarufu kama sangoma ili yaongezeke.
“Wachimbaji wanatakiwa kuwa wavumilivu, kujenga imani na Serikali, taratibu za kutambika zimekamilika ingawa watu wenye imani za kidini waligoma, lakini haikuzuia kufanya matambiko kwenye maduara mengine,” amesema.
Mchimbaji mdogo, Benjamin Mashishi amesema halmashauri ilijisahau kwani ilipaswa kuchukua hatua hiyo kabla ya kuwaruhusu kuanza uchimbaji.
Muumuni wa Kanisa la Ufunuo, Leticia Henry amegoma duara lake namba 26 A kufanyiwa tambiko na waganga hao kutokana na imani yake ya dini kutoruhusu.
“Dhahabu na mafanikio ya utajiri wa kweli hutoka kwa  Mungu siyo shetani, imani yangu ya Kanisa la Ufunuo hainiruhusu kufanya matendo kama hayo kwenye duara langu na sitakubali hata siku moja. Nitapata kwa imani ya Mungu,” amesema Henry.
CHANZO - MWANANCHI

Comments