Featured Post

TANZANIA NI YETU


By WINFRID LUOGA

Mapema Oktoba 2015, Tanzania iliingia kwenye ungwe mpya ya matarajio, shauku, hamu, imani, mategemeo na kiu ya kuona inajiokoa na kujikomboa toka nchi iliyopotoka katika ulimwengu kwenda nchi okovu yenye maendeleo ya viwanda, haki, na yenye furaha. Hii ndio Tanzania iliyokuwa imeahidiwa mnamo mwaka 2015. Kulingana na matarajio ya wananchi, Tanzania ya sasa ni kama ifuatayo:


1. Serikali inayotumikia watu. Kutumikia watu sio tu kuwa na viongozi wanaotawala wengi, kutumikia watu inamaana ya kutoa huduma kwa watu wake. Elimu bora, sio tu elimu bure, kudumisha maadili ya kiubinadamu, kutoa fursa kwa jamii, miundombinu na vitu vingine kadha wa kadha. Hii ndio serikali makini. Kama haitoi elimu stahili, kama haitengenezi fursa kwa watu wake, kama haitoi huduma nzuri kwa watu wake, basi hii sio serikali tuliyoitegemea na hili kama kuna mtu atapinga basi ni mnafiki na ujinga uliopitiliza kwa mtu mwenye akili timamu, makini na mwenye nia njema na mustakabali wan chi na wananchi wake.

John F Kennedy tarehe 11/06/1962 alisema “I would rather be accused of breaking precedents than breaking promises”. Sisi tumegeuza tunasema “I would rather be accused of breaking promises than breaking precedents” halafu utakuta watu wapo mstari wa mbele kushededea. Unashededea nini sasa? Mikopo shida, majanga hayapewi vipaumbele, ajira hakuna na hizi ndo ahadi muhimu zinazomgusa mwananchi moja kwa moja. Utasikia mawaziri wanatuambia “mambo yatakuwa mazuri tu” mazuri! Lini?. If you distance yourself from people then people will distance themselves from you.

2. Serikali ya viwanda. Hili suala limeimbwa sana Tanzania. Kwa nini nasema limeimbwa? Viwanda vimesababisha Tanzania iwe chungu, ihame kwenye matarajio ya wananchi. Hatutaacha kuongeza juhudi zetu ili kuhakikisha maendeleo ya viwanda yanapatikana. LAKINI matatizo na dharula zetu haziwezi kusubiria mpaka Tanzania ya viwanda itimie. Ni sawa na mkeo kuumwa halafu wewe unaacha kumtibia kisa tu unataka kujenga nyumba! Ni kichekesho cha karne. Tumejitahidi sana kufanya mambo na kupambana lakini tunatoa sacrifice isiyostahili ambayo haitasahaulika hata kama Tanzania ikaja kuwa kama UK.
Hawa watu tunaowatesa leo hii ipo siku watatuuliza na watatudai pakubwa na tutashindwa cha kuwalipa! Tetemeko linatokea tunawaza viwanda zaidi. Ajira hakuna tunawaza viwanda zaidi. Mikopo haitoshi tunawaza viwanda zaidi. Halafu ukihoji, utaambiwa serikali inatengeneza mazingira tu. Sasa jiulize inatengeneza mazingira kwa nani? Kwa mtanzania au kwa wao wenyewe? Katika kitabu "A preface to politics" kuna kamsemo kanasema “I favor as a practical policy putting first things first. I shall spare no effort to restore world trade, but the emergence at home cannot wait on that accomplishment”. Sisi emergence zetu tumeziweka kapuni zisubirie viwanda kwanza.

3. Tanzania imejaa unafiki. Vijana tumekuwa wanafiki. Tutajengaje nchi kama tunakuwa wanafiki! Hatuwezi kuijenga nchi katika misingi ya unafiki. Katika kitabu “A preface to politics” kinasema “the best servants of the people must whisper unpleasant truths in the master’s ear”. Tanzania imekuwa na servants ambao hawana ujasiri wa kusema ukweli hata kama una maslahi kwa taifa na vizazi vijavyo. Na ndio maana hatuendi mbele kimaendeleo. Penye unafiki hapawezi kuwa na maendeleo na kama yatakuwepo basi ni ya kinafiki. “we are trying to ignore the society and box them up, and surely they might burst forth destructively in the future and harm our pride.

4. kuinyoosha nchi. Hili kweli ni suala la muhimu sana. Nchi lazima ikae kwenye mstari. Swali ni kwamba inanyooshwaje? Lilianza suala la watumishi hewa, limekuja uhakiki wa vyeti, wanafunzi hewa, mikopo hewa, n.k. mambo mengine yalisimamishwa kwa vigezo hivyo. Mh rais na serikali ya tano kwa ujumla ni suala la kupongezwa kwa mshikemshike huu. Tatizo linakuja pale mazoezi haya yanapogoma kuwa na mwisho! Hakuna kisichokuwa na mwisho. A preface to politics kinasema “it is better to catch the idol-maker than to smash each idol. It would be an endless task to hunt down all the entire mask and the shadows which divert us from our real purpose”.  Hiki kimeshatokea Tanzania tayari. Malengo yetu na ahadi zetu tumeziweka pembeni na kuanza kukimbiza hewa hewa hewa badala ya kutengeneza mazingira ya hizi hewa kutotokea tena.

Na ukweli ni kwamba tunapokubali wazo, tamko, na agizo kama mamlaka badala ya kama nyenzo au njia ya kufikia malengo, tayari tunatengeneza hewa nyingine. Tutaendelea kutengeneza matatizo badala ya kutatua kama tutaendelea kupokea maagizo kama mamlaka badala ya kuyapokea kama njia ya kukamilisha malengo. Ukipokea agizo kama mamlaka,hutaweza kuhoji uhalali, uhalisia na umuhimu wake katika kile kinacholengwa kutokea.

Ni ujinga wa karne kupretend kwamba ukweli ni kitu kingine wakati unaujua. Na ujinga huu upo kwa watu wazembe kureason na wanaogubikwa kwa tama ya mamlaka na kutetea vyeo au kujipendekeza kutaka kupewa vyeo. Na huku kupeana vyeo kwa njia ya kujipendekeza ndiko kunakoleta matatizo katika jamii. Kuhoji ni njia pekee ya kuleta maendeleo popote pale, na mkanganyiko pekee ndio wenye uwezo wa kuleta maendeleo butu.

By
WINFRID LUOGA
Tel: 0756624248/0653363858
Email: wluoga@gmail.com

Comments