Featured Post

RC SINGIDA AAHIDI KUREJESHA SHAMBA LA SAGARA LENYE EKARI ZAIDI YA ELFU TANO KWA WANANCHI

Gari la Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Mhandisi Mathew John Mtigumwe likisukumwa na wananchi wa kijiji cha Sagara baada ya kushusha neema kwa wakazi hao kwa kitendo cha kuwamilikisha shamba la ekari 5,430. Wananchi hao kwa miaka mingi wamekuwa wakitozwa shilingi elfu 30 kwa ekari moja katika msimu wa kilimo. Ushuru huo kwa msimu huu ulipandishwa hadi shilingi 40,000 kwa ekari. Kwa sasa hawatalipa tozo hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Mhandisi Mathew John Mtigumwe akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na umati mkubwa wa watu kijiji cha Sagara na vijiji jirani juzi. Mheshimiwa Mhandisi Mtigumwe ameagiza wakazi wa kijiji cha Sagara watumie shamba linalomilikiwa na halmashauri ya Singida bila kubughuziwa wakati anaendelea na taratibu ya kufuta umiliki wa shamba hilo na halamshauri ya wilaya ya Singida.
Mbunge wa jimbo la Singida kaskazini Mhe. Lazaro Samwel Nyalandu akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na umati mkubwa wa kijiji cha Sagara kata ya Ngimu. Pamoja na mambo mengine Mhe Nyalandu aliiomba serikali ingalie uwezekano wa kuwakabidhi wananchi wa kijiji cha Sagara shamba lenye ukubwa wa ekari 5,430 ambalo halmashauri ya wilaya ya Singida imeshindwa kuliendeleza.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Mheshimiwa Martha Mlata (wa pili kushoto) pamoja na mbunge wa jimbo la Singida kaskazini Mheshimiwa Lazaro Samwel Nyalandu wakijumuika na kikundi cha uhamasishaji cha kijiji cha Sagara kuburudisha wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara juzi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Singida Martha Mlata akitoa nasaha zake kwenye mkutano wa hadhara kijiji cha Sagara ulioitishwa na Mkuu wa mkoa wa Singida Mheshimiwa Mhandisi Mathew John Mtigumwe ili aweze kuongea na wananchi hao. Mlata ameahidi chama cha CCM kitasimamia kikamilifu utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ili iweze kutekelezwa kwa wakati.

Comments