Featured Post

NSSF YAPANGISHA JENGO LA GHOROFA 32 KUWA HOTELI


Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara amesema jengo hilo lipo katika mtaa wa India na Azikiwe jijini Dar es Salaam.

By Raymond Kaminyoge, Mwananchi
Dar es Salaam.
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeingia mkataba ili kupangisha jengo lake la ghorofa 32 kwa ajili ya hoteli ya nyota tano.


Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara amesema jengo hilo lipo katika mtaa wa India na Azikiwe jijini Dar es Salaam.
Makubaliano hayo yalifanywa kati yake na Mtendaji Mkuu wa Icon Hotel Group Africa, Fred Maina.
Alisema mbali na hoteli hiyo,jengo hilo litapangishwa kwa ajili ya mabenki,maduka na nyumba za kuishi.
"Tuna furahi kuanza kupata wapangaji kabla ujenzi haujamalizika,"alisema.
Kwa upande wake mpangaji huyo alisema  hoteli hiyo ya nyota tano itakuwa na nembo ya Best Western Premier ambao ni mtandao wa hotel bora duniani
CHANZO - MWANANCHI

Comments