Featured Post

NCHI ZA AFRIKA ZATAKIWA KUWA NA DATA SAHIHI ZA KILIMO



Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Sekta ya Kilimo Dkt. FlorensTuruka akizindua Warsha ya siku Tano ya Kukusanya Takwimu Sahihi Zinazotokana na Kilimo Barani Afrika, Warsha hiyo imeshirikisha jumla ya nchi 25 na imefunguliwa jijini Dar es Salaam leo (jana). (Picha zote na Benjamin Sawe-Maelezo).

 Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dr. Albina Chuwa akiongea na washiriki wa Warsha ya Siku Tano ya Kukusanya Takwimu Sahihi Zinazotokana na Kilimo Barani Afrika, Warsha hiyo imeshirikisha jumla ya nchi 25 na imefunguliwa jijini Dar es Salaam leo (jana). (Picha zote na Benjamin Sawe-Maelezo).
 Baadhi ya Washiriki wa Warsha ya kukusanya Takwimu Sahihi zinazotokana na Kilimo Barani Afrika wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Sekta ya Kilimo Dkt. Florens Turuka (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo (jana). (Picha zote na Benjamin Sawe-Maelezo).
Baadhi ya Washiriki wa Warsha ya kukusanya Takwimu Sahihi zinazotokana na Kilimo Barani Afrika wakijadiliana jambo baada ya Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Sekta ya Kilimo Dkt. Florens Turuka kufungua warsha hiyo jijini Dar es Salaam leo (jana). (Picha zote na Benjamin Sawe-Maelezo).

Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Tanzania Dkt. Tonia Kandiero akiongea katika uzinduzi wa Warsha ya Siku Tano ya Kukusanya Takwimu Sahihi Zinazotokana na Kilimo Barani Afrika. (Picha zote na Benjamin Sawe-Maelezo)

Benjamin Sawe-Maelezo
Serikali imesema pamoja na umuhimu wa kilimo bado kuna changamoto ya kuwa na data za kuaminika kwa uundaji, ufuatiliaji na utekelezaji wa sera za kilimo.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk. Florens Turuka jana jijini Dar es salaam alipofungua warsha ya siku tano iliyowashirikisha wawakilishi kutoka nchi 25 Barani Afrika ambao utajadili namna ya kuweka mikakati itakayowawezesha kupata data sahihi za kilimo.
“Bado tuna tatizo la Data au Takwimu ambazo tunaweza kuwa na uhakika nazo, hivyo wenzetu wameamua kuweka mikakati itakayosaidia  nchi za Afrika kukusanya Data zitakazosaidia kufanya maamuzi katika sekta ya kilimo na maendeleo vijijini” alisema.
Alisema kilimo kinachangia asilimia 35 ya pato la taifa na asilimia 70 ya ajira na ukuaji wa kila mwaka wa kilimo unatarajiwa kukua kwa asilimia 4.
Wakati huohuo, Meneja wa Takwimu za Kilimo Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Titus Mwisomba alisema bila takwimu hizo hawawezi kupima maendeleo waliyofikia hasa kwa upande wa sekta ya kilimo.
Alisema Ofisi ya Taifa ya Takwimu wamejipanga kutumia teknolojia ya kisasa zikiwemo simu za mkononi ili kupata takwimu kwa haraka na kwa wakati sambamba na kupunguza gharama za uendeshaji wa tafiti mbalimbali nchini.
Alizitaja changamoto zinazowakabili ni pamoja na upatikanaji wa wataalam wa ukusanyaji wa takwimu ambapo tayari wameanza kutoa mfunzo kupitia Chuo cha Afrika Mashariki cha Takwimu ili kukabiliana na changamoto hiyo.
Mbali na kuwashirikisha wataalam mbalimbali, mkutano huo pia uliwashirikisha wataalamu kutoka Shirika la Chakula na Kilimo Duniani(FAO) pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika(AfDB).

Comments