Featured Post

KIMENUKA TENA TRA; RAIS MAGUFULI AMTUMBUA MWENYEKITI WA BODI

Bernard Mchomvu, ambaye uteuzi wake umetenguliwa leo hii.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli, leo hii Novemba 20, 2016 ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania - TRA - Bernard Mchomvu.

Mbali ya kutengua uteuzi wa Mchomvu, Rais Magufuli pia ameivunja bodi hiyo na uteuzi wa mwenyekiti mwingine wa bodi pamoja na bodi yenyewe utatangazwa baadaye.





Comments