Featured Post

ESRF YAFANIKISHA MKUTANO WA 5 WA MWAKA, WAJADILI UCHUMI

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Ashatu Kijaji akihutubia katika mkutano wa tano wa mwaka wa ESRF wa kujadili sera za jamii na mahusiano yake kwenye mabadiliko ya kiuchumi nchini Tanzania ulioandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) jijini Dar es Salaam.(Picha na Said Khalfan wa KVS Blog)

Imeleezwa kuwa ili kumwezesha kila mwananchi wa Tanzania kupata maendeleo na kuondokana na janga la umaskini, Serikali haina budi kutunga sera ambazo zitamgusa kila mwananchi na kuwa na faida jambo ambalo litawasadia kukuza uchumi wao binafasi na taifa kwa ujumla.

Hayo yamesemwa katika mkutano wa tano wa mwaka wa kujadili sera za jamii na mahusiano yake kwenye mabadiliko ya kiuchumi nchini Tanzania na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Philemon Luhanjo katika mkutano wa siku moja wa kujadili sera za kijamii zinavyoweza kusaidia kubadilisha uchumi wa Tanzania, mkutano ambao uliandaliwa na ESRF.

Luhanjo alisema ni vyema Serikali inapokuwa inatunga sera ihakikishe zinakuwa na faida kwa wananchi ili ziweze kuwasaidia kupata maendeleo na kuboresha maisha yao na hata wakati nchi ikielekea katika uchumi wa kati kila mwananchi ahusike na mabadiliko hayo.

"Sera zipo nyingi, zipo za maendeleo ya jumla, elimu, afya, kilimo, viwanda na kila kitu, sisi tunajaribu kuangalia tunapotengeneza sera mbalimbali tuhakikishe kwamba sera hizo zitamnufaisha binadamu, kwamba chochote unachofanya kiwe nikwa faida ya mwanadamu, mipango na malengo yote yawe yanamlenga binadamu kuondoa matatizo yake,

"Serikali inapofanya mipango inatakiwa kupanga mipango ambayo inajaribu kujibu kero za mwananchi, kama ni elimu, kama ni afyaa au kama ni kilimo cha kisasa, tunapotengeneza sera tuwe tunauwianisha, hizo sera zikitekelezeka na mteja wa bidhaa awe ameandaliwa ili mkulima asiwe amepoteza nguvu bure," alisema Luhanjo na kuongeza.

"Tunazungumzia nchi ya viwanda, viwanda gani? na nchi yetu niya kilimo kwahiyo tunatarajia viwanda vingi vitakuwa ni vya kilimo, kwahiyo tunataraji mkulima mdogo aimalishwe ili aweze kuzalisha mazao yanayokwenda kiwandani ni lazima sera ziwe na uwiano mzuri."

Nae Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji alisema Serikali inafahamu kuwa nchi haiwezi kupiga hatua bila kuhusisha mwananchi mmoja mmoja na inachofanya kwa sasa na kuwashawishi watu wenye viwanda kutumia malighafi ambazo zinazalishwa nchini ili wakulima nchini wafaidike na uwepo wa viwanda nchini.

"Tunaamini hatuwezi kuwa na uchumi unaokua kama hali ya kijamii ya wananchi haikui na hata Rais Magufuli alikuwa akisema tangu akiwa katika kampeni kwamba Tanzania ya Magufuli niya viwanda, na viwanda hivi ni kwa ajili ya watu wetu,

Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini wa ESRF, Philemon Luhanjo, akizungumza katika mkutano wa tano wa mwaka wa kujadili sera za jamii na mahusiano yake kwenye mabadiliko ya kiuchumi nchini Tanzania ulioandaliwa na ESRF.

"Kwenye mpango wetu wa miaka mitano tumesisitiza maendeleo ya viwanda lakini vinavyotumia malighafi zinazozalishwa hapa nchini katika kilimo chetu, kwahiyo hatuwezi kuwa na viwanda kama kilimo hakijaendelea, hatuwezi kuwa maendelo ya kijamii kama kilimo chetu hakijaendelea, kilimo ndiyo uti wa mgongo wa taifa letu, kwahiyo tumejadili hilo ili kuona wananchi wetu wananufaika vipi," alisema Kijaji. Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida alizungumza kuhusu mkutano huo ambao umedhaminiwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na kusema,"ESRF kwasasa hivi tupo kwenye mchakato wa kutengeneza Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya mwaka 2017, "Katika hiyo ripoti tumeweza kutaharisha ripoti 11 ambazo zitachangia katika utayarishishaji wa hiyo ripoti na dhumuni kubwa ni kuweza kuzijadili hizo ripoti na kupata uelewa mpana ni kwa kiasi gani sera za kijamii zina mchango mkubwa katika kuleta mageuzi ya kiuchumi hapa Tanzania." 
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akitoa maelezo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi katika mkutano huo.
Mkuu wa Programu, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, Amon Manyama akizungumza katika mkutano wa tano wa mwaka wa kujadili sera za jamii na mahusiano yake kwenye mabadiliko ya kiuchumi nchini Tanzania.
Mtafiti mshiriki mwandamizi wa ESRF, na mashauri wa ufundi wa mradi wa THDR Profesa Marc Wuyts, akiwasilisha mada Situating social policy transformation: A conceptual framework, kwenye mkutano wa tano wa mwaka wa kujadili sera za jamii na mahusiano yake kwenye mabadiliko ya kiuchumi nchini Tanzania.
Mhadhiri wa Masuala ya Afrika na Maendeleo katika Chuo Kikuu cha Edinburgh, Shule ya Sayansi ya Siasa nchini Uingereza Dk.Hazel Gray, akiwasilisha mada yake kuhusu mabadiliko katika sera za kijamii kwenye mkutano wa tano wa mwaka wa ESRF.
Mchokoza mada kutoka taasisi ya Daima na Mtafiti mwandamizi mshiriki ESRF, Profesa Samwel Wangwe, akitoa maelezo yake kuhusu mada iliyowasilishwa mezani kwa wajumbe.
Profesa wa uchumi DoE, Chuo kikuu cha Dar es Salaam Profesa Humphrey Mushi, akiwasilisha mada kuhusu historia ya sera ya jamii katika mkutano huo.
Mgeni rasmi Dk. Kijaji, (wa pili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida, (wa kwanza kushoto), Bi Anna, na mwenyekiti wa bodi ya udhamini ya ESRF, Bw Philemon Luhanjo, Mkurugenzi wa Kupunguza Umaskini na Kuinua Uchumi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Anna Mwasha (wa pili kulia) wakipongeza wakati wa mkutano huo.
Wageni waalikwa wakifuatilia mada mbalimbali kwa makini katika mkutano wa tano wa mwaka wa ESRF wa kujadili sera za jamii na mahusiano yake kwenye mabadiliko ya kiuchumi nchini Tanzania
   
Picha ya pamoja ya washiriki, wakuu ESRF, wakiwa na mgeni wa heshima Dk. Kijaji.

Comments