Featured Post

DANGOTE YAFAFANUA KUSIMAMA KWA UZALISHAJI KIWANDA CHA SARUJI

By Mwandishi Wetu, MwananchiDar es Salaam. Uzalishaji katika kiwanda cha saruji cha Dangote kilichopo Mtwara umesimama tangu wiki iliyopita kutokana na hitilafu katika mitambo ya kiwanda hicho.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dangote Tanzania,  Harpreet Duggal amesema mafundi wa kiwanda hicho  wapo katika matengenezo ya mitambo hiyo na kwamba  shughuli za uzalishaji zitarejea katika siku chache zijazo.
Duggal ambaye amesema kiwanda hicho kilianza uzalishaji wa saruji mapema mwaka huu, amebainisha kuwa kama ilivyo kwa kiwanda kingine kama hicho jambo lolote linaweza kutokea hasa katika miezi ya mwanzo.
Hata hivyo, Ofisa huyo amesema hitilafu hizo  ni za kawaida.
Tangu kuzinduliwa kwa kiwanda cha saruji cha Dangote, bei ya saruji nchini Tanzania imeshuka kwa zaidi ya asilimia 30.
CHANZO - MWANANCHI

Comments