Featured Post

SIMBA CEMENT YAZIPIGA TAFU SHULE TATU TANGA KUPUNGUZA KERO YA MADAWATI




KUFUATIA Uhaba wa madawati katika shule za msingi halmashari ya jiji la Tanga na wanafunzi kusomea chini, Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement kimetoa madawati 100 kwa shule tatu.
Shule hizo ambazo zimefaidika na mpango huo ni Magaoni, Kiruku, Mkombozi na Martini Shamba zote za halmashauri ya jiji la Tanga.
Akizungumza wakati wa makabidhiano mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Tanga , Thobias Mwailapwa, Mkuu wa Idara  Rasilimali watu kiwabda cha Saruji , Diana Malambusi amesema msaada huo umekuja baada ya kuona kero ya wanafunzi kusomea chini kutoisha.
Akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano, Mkuu wa Wilaya, Thobias Mwailapwa, amekishukuru kiwanda hicho (Simba Cement)  na kuyataka mashirika na taasisi pamoja na makampuni kuiga mfano huo ili kumaliza kero ya wanafunzi kusomea chini.
Kwa upande wake Afisa elimu shule ya msingi jiji , Khalifa Shemahonge, amesema madawati hayo yatatumika kama inavyokusudiwa na kuahidi kuyatunza ili kuongeza uelewa  wa  wanafunzi darasani.
                                                     
 



 Mkuu wa Idara ya Rasilimali watu kiwanda cha Tanga Cement (Simba Cement), Dianna Malambugi (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias  Mwailapwa, madawati 100 kwa  shule tatu za msingi, Magaoni, Kiruku, Mkombozi na Martin Shamba  za halmashauri ya jiji la Tanga kupunguza uhaba wa madawati na wanafunzi kusomea chini.



 Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwailapwa, akimkabidhi Afisa Elimu Shule ya Msingi halmashauri ya jiji la Tanga, Khalifa Shemahonge madawati 100 kwa shule tatu ya, Magaoni, Kiruku,  Mkombozi na Martin Shamba yaliyotolewa na kiwanda cha Saruji cha Simba Cementi kupunguza uhaba wa madawati kwa shule hizo.

 Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwailapwa mwenye suti bluu (katikati) na Afisa Elimu shule ya msingui halmashauri ya jiji la Tanga, Khalifa Shemahonge (kulia) wakiwa na wafanyakazi wa kiwanda cha Simba Cement mara baada ya makabidhiano ya madawati 100 kwa shule tatu za halmashauri ya jiji la Tanga .
Walimu wa shule za msingi Magaoni, Kiruku, Martin Shamba na Mkombozi wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Tanga na wafanyakazi wa kiwanda cha Saruji cha Simba Cement mara baada ya makabidhiano ya madawati 100 kwa shule hizo.
Habari hii ni kwa hisani ya blog ya kijamii ya tangakumekucha 0655 90292

Comments