Featured Post

MAKAMU WA RAIS MHE.SAMIA AKUTANA NA MAKUNDI YA MBALI MBALI YA WAKAZI WA MJI WA DODOMA WANAOENDESHA SHUGHULI ZENYE MAHUSIANO NA MAZINGIRA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Makundi mbalimbali ya Wakazi wa Dodoma ambao shughulizao zinahusiana na mazingira kwenye mkutano uliofanyika ukumbi wa Jengo la Hazina ndogo, Makulu mkoani Dodoma ambapo alisisitiza dhambi ya kuharibu mazingira haisameheki hivyo kuwataka kila mmoja awe mstari wa mbele katika kutunza mazingira.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Makundi mbalimbali ya Wakazi wa Dodoma ambao shughulizao zinahusiana na mazingira kwenye mkutano uliofanyika ukumbi wa Jengo la Hazina ndogo, Makulu mkoani Dodoma.
 Vijana wa DOYODO ni sehemu ya makundi yaliohudhuria mkutano wa Makamu wa Rais mjini Dodoma.
 Wazee Mashuhuri wa mji wa Dodoma ni miongoni mwa waliohudhuria mkutano na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Dampo la kisasa lililopo Chidaye ambalo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan alitembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa dampo hilo.
 Kaimu Mkuu wa Idara ya Mazingira na Taka ngumu wa Manispaa ya Dodoma Bw. Barnabas Faida (kushoto) akielezea utaratibu utakaotumika wa kutupa taka katika dampo la kisasa la Chidaye kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye alitembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa dampo hilo ambalo linatarajiwa kuanza kutumia mwezi novemba.
Mhandisi wa Majengo Bi. Gladness Pesha akimuelezea Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan mgawanyo wa ofisi katika jengo la Mkuu wa mkoa wa Dodoma.
  Jengo la Ofisi ya Mkoa wa Dodoma lililopo eneo la Makulu ambalo lipo kwenye hatua za mwisho za kukamilika.

                                      .................................................................
MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan, ametaja vigezo vinavyokwamisha Dodoma kuwa Jiji ikiwa ni pamoja na uharibifu wa mazingira na uzembe wa ukusanyaji mapato.

Kauli hiyo aliitoa jana alipokuwa akizungumza na wazee, wafanyabiashara, vikundi vya usafi wa mazingira na viongozi mbalimbali wa serikali, mjini hapa.

Alisema serikali inapohamia Dodoma lazima kuwe Jiji na ili kupata hadhi hiyo mambo mengi yanahitajika ikiwa ni pamoja na usafi wa mazingira.

Samia alisema mkoa huo umeathiriwa sana na mabadiliko ya tabia nchi ambayo kwa asilimia kubwa yamesababishwa na shughuli za kibinadamu kwa kukata miti ovyo na kuifanya Dodoma kubadilika tofauti na ilivyokuwa awali.

“Wakati nakuja Dodoma mwaka 2002 kulikuwa na baridi sana nakumbuka wakati ule kwa nyumba za zamani ambayo hata ninayoishi kwasasa hazikuwa na kiyoyozi na feni zenyewe zilipachikwa tu hazitumiki maana hali ya hewa ya Dodoma haihitaji kiyoyozi lakini kwasasa joto lipo na baridi ipo ya msimu,”alisema Samia

Comments