Featured Post

GLOBAL ILIPOWATEMBELEA WAFUNGWA GEREZA LA UKONGA DAR ES SALAAM

tamasha-la-wafungwa-13
Mkurugenzi wa Global Publishers, Eric Shigongo (aliyesimama), akiwasalimia wafungwa (hawapo pichani) wa gereza la Ukonga katika Tamasha la Kuadhimisha Siku ya Nyerere (Nyerere Day) Oktoba 14, Ijumaa iliyopita jijini Dar es Salaam.
eric-shigongo
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza Dkt. Juma Malewa akitia saini kitabu cha wageni gerezani Ukonga katika Tamasha la Michezo wakati wa kuadhimisha Nyerere Day. Kutoka kulia ni Mkuu wa Gereza la Ukonga Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Stephen Mwaisabila, Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu, Thom Nyanduga, Mkurugenzi wa Global Publishers Eric Shigongo na Abdalah Mrisho ambaye ni Meneja wa Global Publishers.
tamasha-la-wafungwa-15Baadhi ya wafungwa walioshiriki katika mchezo wa kukimbia kwa magunia katika tamasha hilo.
tamasha-la-wafungwa-16Mmoja wa wafungwa walioshiriki katika mchezo wa kukimbia na yai katika kijiko.
tamasha-la-wafungwa-17Sehemu ya wafungwa walioshiriki katika mchezo wa kukimbia mita 100.
tamasha-la-wafungwa-18Wafungwa walioshiriki katika mchezo wa kuvuta kamba.
tamasha-la-wafungwa-2Hapa ni mchezo wa kushikana mieleka.
tamasha-la-wafungwa-12Eric Shigongo (wa pili kulia) aliyekuwa mgeni rasmi, akisalimiana na wachezaji wa soka wa timu ya Tailors kabla ya mchuano mkali ulioshuhudia timu ya Bush ikiishinda Tailors kwa penalti baada ya kutoka sare ya 2-2.
tamasha-la-wafungwa-4Shigongo akisalimiana na wachezaji wa timu ya Bush kabla ya mchuano wa soka.
tamasha-la-wafungwa-6
...Viongozi meza kuu wakifurahia jambo.
tamasha-la-wafungwa-7
Sehemu ya zawadi zilizoletwa na Global Publishers.
tamasha-la-wafungwa-8
Baadhi ya viongozi wa Jeshi la Magereza na wageni mbalimbali wakishiriki chakula cha mchana pamoja na wafungwa (hawapo pichani).
tamasha-la-wafungwa-9Baadhi ya wachezaji wa timu iliyoibuka mshindi (Bush) wakishangilia baada ya kupachika bao la kusawazisha katika dakika mbili za mwisho na kufanya mchezo kuwa 2-2.tamasha-la-wafungwa-10
Nahodha wa timu iliyoshinda, Johnson Nguza (Papii Kocha) akibeba kombe kwa niaba ya timu yake (Bush) baada ya kulipokea kutoka kwa Eric Shigongo.
tamasha-la-wafungwa-11
Johnson Nguza aka Papii Kocha (wa pili kushoto) akitumbuiza na wanamuziki wa Twanga Pepeta wakati wa tamasha hilo.
tamasha-la-wafungwa-5
Timu ya Bush walioibuka washindi.
Katika kuadhimisha miaka 17 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere, Gereza Kuu Ukonga kwa kushirikiana na Kampuni ya Global Publishers limefanya tamasha la michezo mbalimbali kwa wafungwa wa gereza hilo.
Akiongea katika tamasha hilo, Mkurugenzi wa Global Publishers aliyekuwa pia mgeni rasmi, Eric Shigongo, amewaambia wafungwa kuwa dhamra ya ujio wao gerezani hapo ni katika kuonyesha kuwathamini, kuwahurumia na kuwatia moyo kwamba kuwa kwao gerezani siyo kwamba wametengwa na dunia.
Shigongo aliwatia moyo wafungwa hao kuwa hawatakiwi kukata tamaa na bado wanayo nafasi ya kubadilika na kuwa raia wema.
“Kila mwanadamu anao wajibu wa kubadili maisha yake, Mwalimu Nyerere tunayemuadhimisha leo alizaliwa kama mimi na wewe na kutengeneza maisha yake na leo tunamkubuka, kwa nini wewe ushindwe?” aliuliza Shigongo.
Aliongeza: “Najua wengi wenu mko hapa mkiwa mmeitwa majina mengi kwa kuwa mmehukumiwa, hizi ni hukumu za wanadamu, mnao uwezo wa kuandika kurasa mpya katika maisha yenu na siku mkitoka duniani waseme mtu mwema ameondoka. Siku moja inatosha kubadili maisha yako, kila siku andika ukurasa mpya wa maisha yako na Mungu atakuongoza."
Wadau wengine walioungana na Global Publishers katika tukio hilo ni pamoja na Tume ya Haki za Binadamu nchini ikiongozwa na mwenyekiti wake Thom Nyanduga na Rajab Maranda (aliyewahi kuwa mfungwa gereza hilo la Ukonga) ambao kwa pamoja walileta zawadi mbalimbali kwa wafungwa hao vikiwemo vifaa kama sabuni, soda na kikombe ambacho kilitolewa kwa timu iliyofanya vizuri katika mpira wa miguu.
Katika tamasha hilo wafungwa walishiriki michezo ya kukimbia katika magunia, kukimbia na yai katika kijiko, mbio za mita 100 vijana kwa wazee, mita 400 kupokezana vijiti, kuvuta kamba, mieleka, mpira wa miguu, mashairi, kuonesha vipaji vya uchekeshaji, kuimba kwa mtindo wa kufokafoka, ngoma za jadi na burudani kwa kushirikiana na baadhi ya wanamuziki wa bendi ya Twanga Pepeta.

Picha zote na ASP Deodatus Kazinja wa Jeshi la Magereza.

Comments