Featured Post

AJALI ZA BARABARANI ZAENDELEA KUUA NA KUACHA MAJERUHI MKOANI MWANZA.

Baada ya Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani kufanyika Kitaifa mkoani Geita kuanzia Septemba 29 hadi Oktoba Mosi Mwaka huu, Maadhimisho kama hayo kwa mkoa wa Mwanza yamezinduliwa hii leo kwenye Uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza ambapo imeelezwa kwamba bado juhudi za kila mtumiaji wa barabara zinahitajika ili kutokomeza ajali za barabarani.
Kamanda wa Kikosi cha usalama barabarani mkoani Mwanza, Robert Hussein, amebainisha kwamba kwa kipindi cha mwaka jana kati ya mwezi januari na septemba kulikuwa na ajali 161 zilizosababisha vifo 132 na majeruhi 187 na kwamba kwa kipindi kama hicho mwaka huu kulikuwa na ajali 159 zilizosababisha vifo 150 na majeruhi 162 ambapo takwimu hizo zinaonesha kuwepo kwa ongezeko la vifo 18 sawa na asilimia 12 na upungufu wa majeruhi 25 sawa na asilimia 13.3

Pichani juu ni maandamano ya bodaboda pamoja na wa watumiaji wengine wa barabara yakiingia Uwanjani kwenye maadhimisho hayo ambayo yamezinduliwa na Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella.
Na BMG
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, akizungumza kwenye uzinduzi wa wiki ya usalama barabarani mkoani Mwanza
Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi, akizungumza kwenye uzinduzi wa wiki ya usalama barabarani mkoani Mwanza
Kamanda wa Kikosi cha usalama barabarani mkoani Mwanza, Robert Hussein, akizungumza kwenye uzinduzi wa wiki ya usalama barabarani mkoani Mwanza
Viongozi mbalimbali mkoani Mwanza
Baadhi ya maofisa wa polisi mkoani Mwanza
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella (kushoto) akiteta jambo na Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi (kulia) kwenye uzinduzi huo.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Dkt.Leonald Massale (kulia) kwenye uzinduzi huo.
Mwanahabari Simba Kabonga wa Barmedas Tv akipokea cheti cha utambuzi wa kampuni hiyo katika kutoa elimu ya usalama barabarani
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Waendesha Bodaboda mkoani Mwanza, Seifu Kagoma, akionesha cheti cha utambuzi kwa taasisi hiyo kutoka kwa Kamati ya usalama barabarani mkoani Mwanza.
Wanafunzi wa shule ya Msingi Butimba Jijini Mwanza wakiingia uwanjani kuimba wimbo wa kuhamasisha matumizi sahihi na salama ya barabarani.
Askari wa usalama barabarani mkoani Mwanza, wakitoa elimu ya usalama barabarani kwa baadhi ya wananchi waliohudhuria uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani mkoani Mwanza.
Na George Binagi-GB Pazzo
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, amewataka watumiaji wa barabara mkoani Mwanza, kuzingatia sheria za usalama barabarani jambo ambalo litasaidia juhudi za kupambana na ajali kufanikiwa.


Mongella ametoa kauli hiyo hii leo kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani mkoani Mwanza, uliofanyika katika Uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza, ambapo elimu ya usalama barabarani itaendelea kutolewa kwenye maadhimisho hayo kwa juma zima.

Amesema watumiaji wote wa barabara wanao wajibu wa kufuata sheria za usalama barabarani huku akikemea tabia ya baadhi ya abiria wanaowahimiza madereva kuendesha vyombo vyao kwa mwendo kasi.

Kamanda wa Kikosi cha usalama barabarani mkoani Mwanza, Robert Hussein, amebainisha kwamba kwa kipindi cha mwaka jana kati ya mwezi januari na septemba kulikuwa na ajali 161 zilizosababisha vifo 132 na majeruhi 187 na kwamba kwa kipindi kama hicho mwaka huu kulikuwa na ajali 159 zilizosababisha vifo 150 na majeruhi 162 ambapo takwimu hizo zinaonesha kuwepo kwa ongezeko la vifo 18 sawa na asilimia 12 na upungufu wa majeruhi 25 sawa na asilimia 13.3

Akizungumza kwa niaba ya watumiaji wa barabara, Makamu Mwenyekiti wa Waendesha bodaboda mkoani Mwanza, Seifu Kagoma, amesema kila mtumiaji wa barabara anao wajibu wa kuwa na tahahadhali awapo barabarani badala ya kusubiri wajibu huo kutoka kwa mwenzake.

Maadhimisho ya wiki ya usalama barabarani hufanyika kila mwaka nchini lengo likiwa ni kutoa elimu ya matumizi sahihi na salama ya barabara kwa makundi yote ya watumiaji wa barabara ambapo mwaka huu kitaifa yalifanyika mkoani Geita kuanzia Septemba 29 hadi Oktoba Mosi ambapo kauli mbiu yake ni “Hatutaki ajali, tunataka kuishi salama”.

Comments