Featured Post

VIJANA WATAKIWA KUTUMIA FURSA ZILIZOPO KUJIAJIRI

 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leornad Akwilapo akifungua warsha ya kutengeneza mkakati mmoja kati ya serikali na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu uliondaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) unaofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa NACTE jijini Dar es Saalam. 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Dk Leornad Akwilapo amewataka vijana kutafuta ajira sehemu mbalimbali kwa kutumia fursa zilizopo badala ya kutegemea fursa za serikali.
Kauli hiyo ameitoa wakati akifungua warsha iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO, iliyolenga kuweka mkakati wa pamoja kati ya wadau wa elimu, serikali katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu lengo la nne.

Alisema kwamba ni imani yake kwamba elimu waliyonayo vijana inawaruhusu kufanya shughuli mbalimbali ambazo si lazima kuajiriwa na serikali.

Alisema hakuna nchi duniani ambayo inaweza kuajiri kila mmoja lakini elimu zinazotolewa pamoja na ya Tanzania zinawaandaa vijana kujiajiri wenyewe.

Akizungumzia warsha hiyo alisema kwamba wadau wanakutana kutengeneza mkakati wa pamoja wa kutoa elimu bora kwa wananchi wa Tanzania na namna ambavyo malengo ya maendeleo endelevu (SDG’s) yanavyoshirikishwa katika utoaji elimu.

Alisema lengo la nne la Maendeleo endelevu la Umoja wa Mataifa linasisitiza elimu bora isyokuwa ya kibaguzi kwa watu wote na hivyo mkutano wao ni kuangalia namna wanavyoweza kushirikiana kutoa elimu bora inayowezesha watu wake kujiajiri.

Alisema kwamba mtazamo huo ambao tayari Tanzania ilikuwa nao miaka ya mwanzo ya uhuru ambapo kulikuwa na kisoma cha watu wazima kitu ambacho kilillenga kuwafanya watu kuwa na elimu ya kutosha kuhusu mazingira yao na maisha yao. Naye Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini Tanzania, Zulmira Rodrigues alisema kwamba wameandaa warsha hiyo kwa lengo la kuelezana utoaji bora wa elimu ambao utaendana na matakwa ya sasa ya kumwezesha anayepata elimu hiyo kujiajiri mwenyewe. Aidha amesema lengo la kushirikisha wadau wa elimu ni kuhakikisha kwamba lengo la maendeleo endelevu la nne la Umoja wa Mataifa linashirikishwa katika utoaji elimu kwani lengo hilo ni kuhakikisha elimu kwa wananchi wote bila ubaguzi huku hatua zikichukuliwa katika kuwezesha wanawake kusonga mbele. 

Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues akizungumza kuhusu lake lilivyojipanga kushirikiana na Serikali katika nyanja mbalimbali ya ukuzaji wa elimu haapa nchini.
Mkurugenzi Msaidizi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Makuru Petro akiwasilisha mada wakati wa kongamano lililoshirikisha Serikali pamoja na wadau mbalimbali kujadili ni kwa jinsi gani wanatengeneza mkakati bora ili kuweza kuisaidia serikali kutoa elimu bora na bila ubaguzi wa aina yoyote.Afisa Elimu Mkuu Hilda K. Mkandawire kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia akiwasilisha mada wakati wa kongamano lililowakutanisha wadau mbalimbali wa elimu.Baadhi ya wadau mbalimbali wa sekta ya elimu wakifuatilia kwa makini mkutano uliokuwa unaendelea.Criana Connal kutoka UNESCO akizungumza jambo wakati wa warsha iliyowakutanisha wadau mbalimbali wa elimu ili kujadili mpango mkakati utakaosaidia kuinua kiwango cha elimu nchini Tanzania.Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake (UNWOMEN), Maria Karadenizli (kushoto) akizungumza jambo na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues wakati wa kongamano lililowakutanisha wadau mbalimbali wa elimu.Mkutano ukiendelea.Baadhi ya makundi ya wadau wa sekta ya elimu wakijadiliana ili kutengeneza mpango mkakati wa pamoja kati ya serikali na wadau mbalimbali wa elimu utakaosaidia serikali kutoa elimu bila ubaguzi wa aina yoyote na kwa makundi yote ili kufanikisha lengo namba nne la Mpango wa maendeleo endelevu (SDG’s) linalohusu elimu bora kwa wote.

Comments