Featured Post

UBUNIFU HUU NI VIPAJI, TUVIENDELEZE!

Kila mmoja wetu amepitia katika michezo mbalimbali ya utoto. Kuchezea visoda, kutengeneza magari ya mabati na kadhalika.
Ni michezo ya utotoni ambayo kwa hakika inaakisi utundu na ubunifu ambao mtoto anakuwa nao.


Hata hivyo, wazazi na jamii nzima kwa ujumla huwa haitambui kama huu ni ubunifu na kipaji, tunapuuza tukidhani ni michezo ya watoto kama tulivyozowea.
Lakini kama tungebadilika na kuona kwamba watoto hawa wanaotengeneza hata baiskeli ya miti na kuanza kuindesha wakipakizana kwamba wana vipaji vinavyostahili kuendelezwa, tungewasaidia sana.
Ni wakati wa kutambua vipaji vya watoto wetu na kuviendeleza.

Comments