Featured Post

MITI YA RC MAKONDA ITAOTA JANGWANI AU MSIMBAZI KESHO?



Credit Source: Marco Tibasima

Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini Blog
KESHO Jumamosi Oktoba Mosi, 2016 imetangazwa kwamba ni siku ya upandaji miti kitaifa kwa agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, na wananchi wote wanatarajiwa kuitikia agizo hilo kwa vitendo.
Lakini siku hiyo itakuwa ya pekee kwa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara wakati miamba ya soka nchini, Yanga na Simba, itakapokuwa inamenyana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ukiwa ni mchezo wao wa kwanza kwa msimu wa 2016/17.

Kwa kuzingatia agizo la RC Makonda, ni wazi kwamba asubuhi na mapema Yanga na Simba wanatakiwa waanze kupanda miti katika maeneo yao kabla ya kuelekea Uwanja wa Taifa.
Kupandwa kwa miti ni jambo moja, lakini kustawi ni jambo jingine, na swali la kisanii Zaidi lililopo ni kwamba, ni wapi ambako miti inayohimizwa na RC Makonda itachipua – kwamba dalili njema zinaweza kuonekana pia kwa matokeo ya uwanjani hapo kesho.
Hii maana ama tafsiri yake ni kwamba, ni upande upi ambao kesho utaruhusu bao kuingia kama dalili njema ya kuota kwa miti hiyo?
Matokeo ya uwanjani hapo kesho ni Dhahiri yataleta hadithi nyingine kwa timu hizo mbili, kwani timu itakayoshinda itatafsiriwa kwamba ndiyo iliyokwenda kupanda mti kwa mwenzake!
Tusubiri tuone nani atacheka baada ya majigambo ya muda mrefu.

Comments