Featured Post

MBUNGE WA JIMBO LA SEGEREA BONNAH KALUWA AONGOZA SEMINA YA WANAWAKE WAJASIRIAMALI JIJINI DAR ES SALAAM

 Mbunge wa Jimbo la Segerea,Bonnah Kaluwa (katikati) akiingia kwenye ukumbi wa Nyantale kwa ajili ya kufungua semina ya ujasiriamali ya wanawake eneo la Tabata Bima jijini Dar es Salaam leo.

 Wanawake wa Jimbo la Segerea wakiwa kwenye semina ya ujasiriamali ukumbi wa Nyantale eneo la Tabata Bima jijini Dar es Salaam.
 Wanawake wa Jimbo la Segerea wakiwa kwenye semina ya ujasiriamali ukumbi wa Nyantale eneo la Tabata Bima jijini Dar es Salaam.
 Katibu wa Ofisi ya Jimbo la Segerea,Jacqueline,akizungumza na akinamama wa jimbo hilo kwenye semina ya ujasiriamali.
 Mkufunzi wa Elimu ya Utunzaji wa Fedha kutoka Benki ya Equity,Daudi Mwashilindi,akitoa mada ya utunzaji wa fedha na mpangilio wa mapato na matumizi jinsi inavyosaidia kwa wajasiriamali kukua kibiashara kwenye semina hiyo.

Meneja wa Kanda ya Temeke wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,Erica Sendegeya,akizungumza na wanawake wajasiriamali umuhimu na faida ya kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii kwenye semina  hiyo.
 Mkufunzi wa Kujitegemea,Albert  Magonga,akitoa mojawapo ya mada ya kuwawezesha wanawake wajasiriamali kukua kiuchumi kupitia biashara zao.
 Mkufunzi wa Elimu ya Utunzaji wa Fedha kutoka Benki ya Equity,Daudi Mwashilindi,akitoa mada ya utunzaji wa fedha na mpangilio wa mapato na

 Mama mjasiriamali akichangia mada katika semina hiyo
 Semina ikiendelea.
 Wanawake wajasiriamali wa Jimbo la Segerea wakisikiliza kwa makini wakufunzi waliokuwa wakizungumza kwenye semina ya ujasiriamali ya kuwainua kiuchumi wanawake. 
PICHA ZOTE  na SHUNDA BLOG kwa mawasiliano Email:elisashunda@gmail.com,Simu:0719976633
 Mwenyekiti wa Vikundi vya Wanawake Wajasiriamali wa Jimbo la Segerea,Salma Fumbwe,akibadilishana mawazo na Mbunge wa Jimbo la Segerea,Bonnah Kaluwa (kushoto) katika semina ya ujasiriamali ya wanawake iliyofanyika ukumbi wa Nyantale eneo la Tabata Bima,jijini Dar es Salaam,leo. Kauli Mbiu ni Mwanamke Simama Inuka Piga Kazi”.

 Mbunge wa Jimbo la Segerea,Bonnah Kaluwa,akizungumza na wakinamama wajasiriamali wa jimbo lake kwenye semina ya ujasiriamali kwa wanawake iliyofanyika kwenye ukumbi wa Nyantale,Tabata Bima jijini Dar  es Salaam leo.
 Mbunge wa Jimbo la Segerea,Bonnah Kaluwa,akizungumza na wakinamama wajasiriamali wa jimbo lake kwenye semina ya ujasiriamali kwa wanawake iliyofanyika kwenye ukumbi wa Nyantale,Tabata Bima jijini Dar  es Salaam leo.
 Mbunge wa Jimbo la Segerea,Bonnah Kaluwa,akizungumza na wakinamama wajasiriamali wa jimbo lake kwenye semina ya ujasiriamali kwa wanawake iliyofanyika kwenye ukumbi wa Nyantale,Tabata Bima jijini Dar  es Salaam leo.

Na Elisa Shunda

WANAWAKE washauriwa kutenganisha fedha ya msingi wa biashara na fedha ya matumizi mbalimbali ya nyumbani ili kuboresha na kusonga mbele kiuchumi tofauti na wakichanganya watakuwa wanadumaza biashara zao na matokeo yake kupata hasara inayopelekea kusimamisha biashara anayoifanya.

Hayo yamezungumzwa na wakufunzi mbalimbali waliokuwa wakitoa elimu ya ujasiriamali kwa wanawake kwenye semina yenye ujumbe wa kauli mbiu ya Mwanamke Simama Inuka Piga Kazi iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Segerea,Bonnah Kaluwa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Nyantale eneo la Tabata Bima jijini Dar es Salaam leo.

Akizungumza kwenye semina hiyo mbunge wa jimbo hilo,Bonnah Kaluwa,alisema kuwa ameamua kuandaa semina ya ujasiriamali ya wanawake kwa ajili ya kuwapatia elimu mbambali za ujasiriamali pamoja na elimu ya utunzaji wa fedha za biashara kwenye sehemu yenye uhakika pasipokuwa na shaka wala wizi kwa kuwaletea benki ya Equity na Mfuko wa hifadhi ya Jamii ya PPF ambao watawasaidia kuwahifadhia fedha zao pamoja na kuwapatia bima ya afya na fao la kustaafu endapo watakidhi vigezo.

“Wakinamama nimefurahi kwa jinsi mlivyojitokeza kwenye semina hii natumaini tukimaliza hapa kila mmoja wetu atakuwa amepata elimu ya kutosha kuhusiana na masuala ya ujasiriamali likiwemo la kutofautisha fedha ya matumizi ya nyumbani na fedha ya biashara kwa kuwa ukipata elimu ya kutenganisha vitu hivyo utaendelea kwenye biashara yako huwezi kutoa fedha ya biashara kununua chakula au kumsomesha mtoto lazima utayumba hivyo ni bora kila mtu ategeshe sikio lake vizuri kusikiliza elimu itakayotolewa hapa ambayo itatufumbua kutofautisha masuala ya nyumbani na biashara ambayo itatusaidia sana kufikia kwenye malengo yetu” Alisema Kaluwa

Aidha akitoa elimu ya ujasiriamali kwenye semina hiyo,mkufunzi wa kujitegemea,Albert Magonga,alisema kuwa huwezi kuwa mjasiriamali halafu huweki mazingira ya kuonyesha bidhaa zako kwa majirani yako wanaokuzunguka na pia ni vyema mjasiriamali kuwa mbunifu wa kutambua eneo unaloishi ni kitu gani ambacho ni adimu ili uanzishe upate wateja wako ambao watanunua biashara yako kutokana na jinsi unavyokiandaa.

Naye Mkufunzi wa utunzaji wa fedha kutoka benki ya Equity,Daudi Mwashilindi,alisema kuwa watu wengi wanaokopa fedha katika taasisi mbalimbali nchini wana mapungufu ya kutokuwa na elimu ya fedha jinsi ya kuitumia akatolea mfano benki yao wanakopesha hadi maprofesa ambao wanaaminika wana upeo mkubwa wa kufikiri lakini kutokana na kutokuwa na elimu ya fedha wanashindwa kutumia vizuri fedha walizokopa mwisho wanauza nyumba yake ili kurudisha kiasi cha fedha walizomkopesha.

“Unapotaka kwenda kukopa katika taasisi yoyote ya fedha ni lazima uwe na elimu ya matumizi ya fedha la sivyo utaishia pabaya kwa mfano benki yetu ya Equity tunakopesha hadi maprofesa ambao tunaamini wana upeo mkubwa wa akili ila kutokana na kutokuwa na elimu ya utunzaji na utumiaji wa fedha wanashindwa kurudisha fedha zetu tunauza nyumba yake kwa ajili ya kurudisha kiasi cha fedha tulizomkodisha,hivyo ninyi leo mnapata elimu ya kujua bajeti yako na mapangilio wa mapato na matumaini ikiwemo na daftari la biashara zako ili kujua mahesabu yako” alisema Mwashilindi.

Akaongeza kwa kusema mjasiriamali bora anapaswa kupata taarifa sahihi kutoka kwenye vyombo vya habari ni fursa kwake akatolea mfano ukipata taarifa ya habari kuwa Mkoa wa Dar es Salaam kuwa mwezi wa kumi kutakuwa na joto kali wewe kama mfanyabiashara kutokana na taarifa hiyo lazima apange biashara ya kuuza vitu vinavyoendana na kipindi hicho kwa kufanya biashara kama Soda,Maji na Juice.

Kwa upande wake Meneja wa Kanda ya Temeke wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Erica Sendegeya,aliwashauri akinamama wajasiriamali kujiunga na mfuko huo utakaowasaidia mambo mbalimbali ikiwemo la masuala ya afya kwa kupata vitambulisho vya NHIF kwa bei nafuu na kuwaambia mfuko wa PPF ukichangia kwa takribani miaka 15 kwa kila mwezi shilingi 20000 unaingizwa kwenye fao la pensheni hivyo aliwataka wakinamama hao kujiunga na mfuko huo.

Semina hiyo ya ujasiriliamali kwa wanawake wa jimbo la Segerea itawezesha kuwapatia elimu ya utunzaji wa fedha akinamama zaidi ya 500 ambao wapo kwa kanda mbili ambapo mkutano huu wa mwanzo ulifanyika kwenye jimbo hilo kwa kanda ya A ambapo baadae kanda B nao watapatiwa elimu hiyo kupitia ufadhili wa benki ya Equity na Mfuko wa Hifadhi ya jamii kushirikiana na ofisi ya jimbo la Segerea.

Comments