Featured Post

LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA KUENDELEA WIKIENDI HII


Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inaendelea leo Septemba 30, 2016 kwa mchezo mmoja tu, unaozikutanisha timu za Toto Africans na Ndanda ya Mtwara katika mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Kama ilivyo kwa leo, kesho pia kutakuwa na mchezo mmoja tu utakaowakutanisha watani wa jadi, Young Africans na Simba katika dimba la Taifa, Dar es Salaam. Mchezo huo, umekuwa na hamasa ya aina yake.
Lakini kwa siku ya Jumapili, michezo itakuwa mitano ambako Mbeya City itaikaribisha Mwadui kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya; Majimaji itakuwa mwenyeji wa Stand United kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea wakati African Lyon itakuwa mgeni wa Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Manungu, Mvomero mkoani Morogoro.
Mbao baada ya kucheza na Ruvu Shooting wiki iliyopita, ilibakia Mlandizi mkoani Pwani kusubiri kucheza na JKT Ruvu Jumapili kwenye Uwanja wa Mabatini huko Mlandizi wakati Kagera itaikaribisha Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera.

Comments