Featured Post

HIZI NDIZO TIMU ZILIZOSHIRIKI LIGI DARAJA LA KWANZA DAR ES SALAAM MWAKA 1964



Kikosi cha Cosmos cha miaka ya 1960. Kushoto kabisa ni Mansour Magram.

Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini Blog
KABLA ya kuanza kwa Ligi ya Taifa mwaka 1965, mashindano makubwa kabisa ya soka yalikuwa Ligi Daraja la Kwanza Dar es Salaam yaliyosimamiwa na Chama cha Ligi ya Soka cha Dar es Salaam (DFLA). Chama hiki mwaka 1964 kilikuwa kinaongozwa na Mwenyekiti Abdu Hussein ambaye alichaguliwa tena mwaka huo, Makamu Mwenyekiti J.A. Mwita, Katibu K.R. Mseselo, Mweka Hazina Patrick Masukuzi, wajumbe; Ali S. Ketto, A.M. Tale na Twaha Hassan.

Kwa ujumla, DFLA, ambayo baadaye ndiyo ilikuja kuzaa DRFA, ilikuwa na nguvu sana, na iliendesha ligi ya soka mjini Dar es Salaam kwa miaka mingi sana huko nyuma. Kwa kifupi ilikuwa na nguvu kuliko hata TFA (TFF) yenyewe.
Ligi Daraja la Kwanza Dar es Salaam kuwania Kombe la Percy Brown mwaka 1964 ilishirikisha timu za Yanga, Magomeni, Sunderland Dar, Prisons Dar, Hydra A (baadaye ikaitwa Cargo), Cosmopolitans, PWD, Goans Institute (baadaye Dar Institute), East African Tobacco (baadaye England American Tanzania Tobacco – baadaye Sigara, baadaye Moro United), Aga Khan, Polisi Dar, Canada Dry na Technical College.
Ligi hiyo, kubwa kabisa ya soka kwa wakati huo, mwaka huo ilianza Julai 17 na kushuhudia Cosomopilitans ikitwaa ubingwa na Yanga ikishika nafasi ya pili baada ya kuichabanga Prisons mabao 5-2 katika mchezo wake wa mwisho hapo Oktoba 19, 1964.
Yanga mwaka huo ilikuwa na wachezaji Maganga, Kiwanga, Salum Kikopo, Kivumbi, Ketto, Kamando Zuberi, Mawazo Shomvi, Ali Esso, Vedasto Mulamula, Jacob Popo, Opio, Juma Salum, Kassim Lengwe, Said Waziri, Juma Kibaba, Abdallah Upete, Hangai, Adam, Mohammed Hussein Hassan 'Msomali'. Kocha alikuwa Ali S. Ketto.
Cosmos: Kitwana Manara, Masiku, Mathias Samuel Kisa, Salehe Yahaya, Badru, Mansour Magram, Bona, Hamisi Ali 'Askari', Bakar, Maufi, Ismail Swedi, Chaki, Mbaraka Peter, Owitti, Boi Iddi, Said Karama, Mohammed, Gihigi, Abdulali. Ilikuwa inanolewa na Marijani Shaaban Marijani, kaka wa mwanamuziki Marijani Rajabu Marijani ambao baba zao ni mtu na mdogo wake.
Hydra (Cargo): Abdullah Zonga, Dotto Salum, Alimbe, Said Mohammed Addallah 'Walala', Mustafa Choteka, Abdulrahman Lukongo, Said Kalibaba, Abdallah Salum, Inzi, Dona, Said Juma, Mtoro Ramadhan 'Meja', Mwinjuma Said, Mohammed Masoud, Ochaya Juma, Abdulla Mzee, Thomas Mpepo, Kifimbo, Said Waziri na Ramadhan Mbegu.
Goans: Ivan Almeida, John D'Souza, Edward D'Souza, Dourado, Pereira, Hatibu, Fernandos, Gangy Almeida, Chic Saldanha, na wengineo.
Aga Khan: Karim Jaffar, Sultan Raja, Chaglani, Sadru Janmohamed 'Hichu', Sumar Hussain, Manji (sijui kama ana undugu na Yussuf Manji wa Yanga), Matata, Sadru Kassum, Ghathia, Idat, Paroo, Jamal, Ali Ismail, na wengineo.
Canada Dry: Iddi Ali, Hamadi Kishonde, Mwintanga, Msuba, Abdallah, na wengineo.
Magomeni: Haruna Rashid Mwinshehe, Idd, Ally, Athumani, M. Kondo,
Polisi: Akwitende, Polikapo, na wengineo.
Tobacco: Abdulla Aziz, Badu, Mtumwa Mgeni, na wengineo.
PWD: Shabani Ali, Hatibu Mtoto, Mohammed Njunde, Gulu, Hamisi Fikirini, Juma Mussa, na wengineo.
Prisons: Hamisi, Ekaristi, na wengineo.
Sunderland: Chuli, Hamisi Kilomoni, Tayari Mussa, Mussa Libabu, Abdu Rajab Kibunzi, Ally Durban, na wengineo.
Wakati ule wachezaji wengi walikuwa wakizitumikia klabu za mashirika na taasisi kama Hydra, Tobacco, Prisons na kadhalika, lakini pia walikuwa wakizichezea timu za mtaani kama Yanga, Sunderland na nyinginezo.
Extracted from: UBINGWA WA SOKA TANZANIA, mswada ambao bado kuchapwa.

Comments