Featured Post

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWAPA ‘MTIHANI’ MAOFISA ARDHI SUMBAWANGA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

By Mussa Mwangoka, MwananchiRukwa. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa siku mbili kwa Mkuu wa Idara ya Ardhi na Miundombinu wa Mkoa wa Rukwa na Ofisa Ardhi wa Manispaa ya Sumbawanga kutatua matatizo ya ardhi yanayowakabili wakazi wa maeneo hayo.
Waziri Mkuu alitoa amri hiyo juzi wakati akizungumza na wakazi wa manispaa hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Mandela.
Alisema leo shughuli zote za idara ya ardhi zitasimama na badala yake maofisa watashughulikia kero za wakazi hao  kwa kuwasikiliza na kuangalia namna ya kuzitatua.
“Ijumaa (leo) kuanzia saa tatu asubuhi wenye kero za ardhi wote waende kwenye ukumbi wa manispaa, mkuu wa idara atakuwa na watumishi wote. Mtasikilizwa kero zenu na kupatiwa ufumbuzi,” alisema Majaliwa.
MWANANCHI

Comments