Featured Post

WATANZANIA WALIOSOMA CHINA KUPATA UONGOZI MPYA

By LEAH MUSHI
Chama cha watanzania waliosoma China- China Allumni Association of Tanzania (CAAT) hii leo tarehe 27 August, 2016 kinatarajia kufanya uchaguzi mkuu kwa ajili ya kupata viongozi wake wapya.

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Rombo Green Views Hotel Sinza jijini Dar es Salaam kuanzia saa saba kamili mchana na kufuatiwa na sherehe ya kuwapongeza viongozi wapya na kuwaaga viongozi waliomaliza muda wao.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa uchaguzi wa chama hicho Gustav Sanga uchaguzi huo utawaweka madarakani viongozi hao miaka mitatu kwa mujibu wa katiba ya chama hicho.
Nafasi zinazogombewa katika uchaguzi huo ni Mwenyekiti, Katibu, Mhazini, Mkurugenzi wa Takwimu, Habari, Mkurugenzi wa Sanaa, Utamaduni na Urithi pamoja na Mkurugenzi wa Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Sanga pia amewakaribisha watanzania wote waliomaliza China kujiunga katika chama hicho ili kuweza kutimiza malengo mbalimbali waliyojiwekea ikiwemo kuishauri serikali masuala yahusuyo Tanzania - China.
Chama hicho cha watanzania waliosoma China kina miaka sita tangu kuanzishwa kwake na kina wanachama tangu waliosoma china miaka ya1980 kwa ngazi ya shahada , astashahada na shahada ya uzamivu.

Comments