Robert Lowassa, mmiliki wa kituo cha radio cha Radio 5 kilichoko jijini Arusha
SERIKALI kupitia kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye imevifungia kwa muda usiojulikana vituo vya Radio 5 ya Arusha inayomilikiwa na Robert Lowassa, ambaye ni mtoto wa mwanasiasa Edward Lowassa, na Magic FM
ya Dar es Salaam kwa sababu za uchochezi.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Waziri Nape amesema kuwa vituo
hivyo kwa nyakati tofauti zilitangaza habari ambazo ndani yake zina
uchochezi.
“Adhabu hii ya kuvifungia kwa muda vituo hivyo viwili inaanza leo
(Agosti 29 2016) hadi pale kamati itakapomaliza kazi yake,” alisema
Nape.
Aidha, amesema kuwa ameiagiza Kamati ya Maudhui ya vyombo vya habari
kuviita vyombo hivyo na kuvihoji kwa kina kisha kumshauri hatua zaidi ya
kuchukua.
Comments
Post a Comment