Featured Post

NAFASI 7,000 ZA MASOKO KUGAWIWA WAFANYABIASHARA WADOGO MBEYA

Soko la Mwanjelwa jijini Mbeya

By Lauden Mwambona, Mwananchi
Mbeya. Nafasi 7,000 zimepatikana katika masoko manne ya jijini Mbeya zitakazogawiwa kwa wafanyabiashara wadogo waliokuwa wakipanga bidhaa zao chini kwenye mitaa mbalimbali.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amesema hayo jana alipozungumzia utekelezaji wa agizo lake kwa uongozi wa jiji la kutaka wafanyabiashara wadogo wapewe maeneo ndani ya masoko.
Alisema soko la Mwanjelwa limegundulika kuwa lina meza nyingi zinazoweza kutumiwa na wafanyabiashara hao.
Ofisa Habari wa Jiji la Mbeya, John Kilua alisema masoko mengine ni la Sido, Soweto na Soko jipya la Nanenane .
Wiki iliyopita, Makalla aliuagiza uongozi wa jiji kuwaondoa wafanyabiashara wanaopanga bidhaa zao chini kando ya barabara kuu na vituo vya mabasi vya Kabwe, Nanenane na Stendi Kuu na badala yake wapatiwe maeneo ndani ya masoko.
CHANZO: MWANANCHI

Comments