Featured Post

MASHIRIKA YANAYOBARIKI USHOGA YASHIKWA PABAYA

 Mashoga wakiandamana nchini Uganda.
Wanajamii nao wakaandamana Uganda kupinga ushoga.

By Rachel Chibwete, MwananchiDodoma. Msajili wa mashirika yasiyo ya kiserikali nchini (NGO’s), Marcel Katemba amesema Serikali haitasita kuyafuta mashirika yanayojihusisha na masuala ya kutetea mapenzi ya jinsia moja.
Katemba alitoa kauli hiyo mjini hapa jana baada ya kumalizika Uchaguzi Mkuu wa viongozi wa kitaifa wa NGO’s nchini.
“Kwa mfano hapa nchini hatujasajili shirika hata moja linaloruhusu mapenzi ya jinsia moja, nasema hivyo kwa sababu yanajua kuwa kitu cha namna hiyo hakikubaliki, sasa utakuta mashirika haya yanajiingiza kwenye sakata hilo kutokana na masharti ya kupata fedha yanayotolewa na wafadhili kutoka nje ya nchi, wanaotaka kuunga mkono mapenzi ya jinsia moja.
“Serikali hatujaruhusu mambo hayo nchini, ndiyo maana tukalifuta usajili Shirika la Sisi kwa Sisi na hatutasita kumchukulia hatua atakayejihusisha na mambo yaliyo nje ya katiba yake,” alisema.
Alisisitiza kuwa Serikali italifutia usajili shirika lolote lisilo la kiserikali litakalofanya kazi zake kinyume na katiba ya nchi.
CHANZO: MWANANCHI

Comments