Featured Post

MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AHUDHURIA KIKAO CHA SADC TROIKA MJINI MBABANE SWAZILAND

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akipata maelezo kutoka kwa  Mkurugenzi na Balozi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Innocent Shio (katikati) kulia ni Waziri Mambo ya Njena ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) muda mfupi kabla ya kuanza kwa  Mkutano wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Troika Summit) unaowahusisha Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika umefanyika mchana huu  katika ukumbi wa Grand- Lozitha mjini Mbababe Swaziland.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akijianda na mkutano wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Troika Summit) unaowahusisha Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika umefanyika mchana huu  katika ukumbi wa Grand- Lozitha mjini Mbababe Swaziland.
 Hii ndio muonekano wa Ukumbi wa Mkutano wa Mandvulo Grand uliopo Lozitha mjini Mbabane Swaziland ambapo mkutano wa 36 SADC unafanyika.
                                       ............................................................. 
Mkutano wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Troika Summit) unaowahusisha Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika umefanyika mchana huu  katika ukumbi wa Grand- Lozitha mjini Mbababe Swaziland.

Mkutano huo wa Troika unaohusisha nchi Tatu ambazo ni za Utatu ikiwemo Tanzania, Msumbiji na Afrika Kusini ambapo kwa kuzingatia utaratibu huo mkutano huo unahudhuriwa na Wakuu wa nchi na serikali wa Msumbiji kama Mwenyekiti wa Asasi hiyo (SADC Organ Troika Summit) na Afrika Kusini kama mwenyekiti aliyetoka na Tanzania inatarajiwa kukabidhi uenyekiti wa Asasi hiyo.

Baadhi ya ajenda ambazo viongozi hao watajadili kwenye mkutano huo ni hali ya ulinzi na usalama katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Madagascar na Lesotho, masuala ya upatanishi na utatuzi wa migogoro pamoja na maombi ya Burundi na Comoro kutaka kujiunga katika Jumuiya ya Mandeleo Kusini mwa Afrika- SADC.
Katika mkutano huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anawakilishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Ufunguzi rasmi wa mkutano wa SADC utafanyika terehe 30-Aug-16 katika ukumbi wa  Grand- Lozitha mjini Mbababe Swaziland ambapo pamoja na Mambo mengine mkutano huo utatoa zawadi kwa wanafunzi walioshinda katika uandishi wa insha katika jumuiya hiyo.


Comments