- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Banda la kisasa la sungura ambapo pia mkojo unakingwa ili kuuzwa viwandani.
Nyama ya sungura ikiwa imefungashwa na kuuzwa kwenye maduka makubwa (super markets).
Na Daniel Mbega
WANUNUZI wengi na wasindikaji wa nyama wanapendelea sungura weupe
kwa vile manyoya meupe huwa hayaonekani kirahisi kwenye nyama kuliko manyoya
meusi.
Manyoya meupe pia yanaweza kubadilishwa rangi kwa kutumia dye.
Haijalishi ni aina gani ya sungura, lakini ni lazima uanze nasungura wenye afya njema kutoka kwa muuzaji na mfugaji wa sungura anayeaminika.
Sungura wenye afya njema ni muhimu kwa sababu walio wadhaifu wanaweza kuzaa
watoto wadhaifu pia. Hakikisha unatembelea maeneo kadhaa ya wafugaji wa sungura
kabla ya kununua wale unaotaka kuwafuga.
Usafi na mpangilio wa banda la sungura unaweza kuwa taswira sahihi
ya ubora wa sungura utakaowanunua.
Mabanda mengi ya sungu mara nyingi watu hawaruhusiwi kuingia ovyo
ikiwa ni njia mojawapo ya kuepuka kuleta magonjwa ndani. Kama utatembelea kwa
mfugaji akakwambia huruhusiwi kuingia bandani, tafadhali heshimu uamuzi wake.
Kama mfugaji atakataza kuingia ndani, tafadhali muombe walau
akuruhusu uingie na kuangalia sungura walivyo unaotaka kuwanunua na namna ya
kuwahudumia. Tafadhali usinunue ikiwa hawatakuruhusu kabisa kuingia ndani.
Kama mnunuzi, unapaswa kuwa na haki ya kuona kile unachotaka
kukinunua.
PATA MWONGOZO UTAKAOKUSAIDIA KATIKA UFUGAJI NA JINSI YA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI YAKIWEMO MAGONJWA.
PATA MWONGOZO UTAKAOKUSAIDIA KATIKA UFUGAJI NA JINSI YA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI YAKIWEMO MAGONJWA.
WASILIANA
NA DANIEL MBEGA KWA SIMU HII +255 656 331974 ILI UPATE NAKALA YAKO SASA KWA
GHARAMA NAFUU KABISA YA SHS. 20,000/= TU!! … FUATA LINK HII UPATE MAELEZO
ZAIDI.
Comments
Post a Comment