Featured Post

HIZI NDIZO AINA ZA SUNGURA WANAOFAA KUFUGWA

Sungura aina ya Flemish Giant ambaye anaweza kufikisha hadi kilogramu 10.


Na Daniel Mbega
Katika makala haya tunaangalia aina mbalimbali za sungura ambao wanafaa kufugwa.
Kwa kawaida, mfugaji anahitaji kutambua sungura ambao atatumia kama mbegu kwa kuzalisha wengine wenye ubora wa hali ya juu. Ni vyema kutenga sungura wangali wadogo wakiwa miezi minne kwa wa kike na miezi sita kwa sungura wa kiume, yaani kabla hawajaanza kuzaa.
Baada ya kupandisha kwa mara ya kwanza na wanapopata mimba sungura hao wa kike ni vyema kuwatenga na kuwaweka katika chumba chao maalum ili kuanzisha kizazi kingine.
Kuna aina mbali mbali wa sungura lakini wanagawanywa mara mbili kwa matumizi. Moja ni kwa matumizi ya ngozi yake kwa kutengeneza kofia, mifuko, na mishipi na pili kuna aina ya sungura ambao hufugwa kwa kuzalisha nyama. 
Mfano wa aina ya sungura wa ngozi ni “Angora” ambaye manyoa yake ni marefu. Na kwa wale wanaofugwa kwa nyama ni aina ya sungura ambao hukua haraka, uzito wa sungura wa nyama ni kutoka kilo mbili hadi kilo tano. 
Mtu anaweza kuvutiwa na rangi nyeupe ya manyoya laini kwa sungura kama Angora, lakini hao hawafugwi kwa ajili ya nyama.
PATA MWONGOZO UTAKAOKUSAIDIA KATIKA UFUGAJI NA JINSI YA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI YAKIWEMO MAGONJWA.
WASILIANA NA DANIEL MBEGA KWA SIMU HII +255 656 331974 ILI UPATE NAKALA YAKO SASA KWA GHARAMA NAFUU KABISA YA SHS. 20,000/= TU!! … FUATA LINK HII UPATE MAELEZO ZAIDI.

Comments