- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Dume na jike la Nubia
Jike la Nubia
Na Daniel Mbega
Hapa tutazungumzia aina mbili za
mbuzi wa maziwa jamii ya Nubia. Kwanza kuna mbuzi wa Nubia wa asili ambao kwao
hasa ni Sudan na ukanda wa kusini wa Misri. Mbuzi hawa wa Nubia ndio maarufu
zaidi kwa watengenezaji wa cheese na ice cream kutokana na maziwa yao kuwa na
mafuta mengi kuliko mbuzi wengine.
Mbuzi hawa wako katika rangi
mbalimbali na ndio mbuzi wakorofi zaidi kati ya jamii za mbuzi wa maziwa.
Unaweza kuwatofautisha mbuzi wa Nubia
na jamii nyingine kutokana na uso wao wa duara (maarufu kama pua ya Kirumi) na
masikio marefu yaliyotepeta. Mbuzi jike mkubwa ana uzito wa zaidi ya kilogramu
61 wakati beberu ana uzito wa zaidi ya kilogramu 77. Jike la Nubia linatoa
wastani wa lita 680 za maziwa kwa mwaka yenye kiwango cha asilimia 4 ya siagi.
Halafu kuna mbuzi aina ya
Anglo-Nubia, ambayo huko Marekani wanaiitia Nubia tu. Jamii hii ni chotara
ambao walipatikana nchini Uingereza kutokana mbuzi jike wa asili wa maziwa wa
Uingereza na madume kutoka Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati.
Mbuzi hawa hawana tofauti sana na
Nubia wa asili kwa sababu sifa zao kubwa ni miili mikubwa, masikio makubwa na
marefu yaliyotepeta na pua ya Kirumi.
Kutokana na asili yao ya Afrika
Kaskazini na Mashariki ya Kati ambako kuna jangwa na joto jingi, Anglo-Nubia
wanaweza kuishi katika mazingira ya joto kali na wana msimu mrefu wa kuzaa
kuliko jamii nyingine ya mbuzi wa maziwa.
Anglo-Nubia wanafahamika zaidi kama
mbuzi wa maziwa na nyama pia, lakini ni maarufu kwa maziwa yao ambayo yana
mafuta mengi, ingawa kwa wastani, wanazalisha kidogo kuliko jamii nyingine za
mbuzi hao wa maziwa.
Anglo-Nubia ni wakubwa, ambako jike
linafikisha uzito wa kilogramu 64 wakati dume linaweza kufikisha hadi kilogramu
90.
Wastani wa kimo kwa mbuzi hawa wa maziwa
wakipimwa ni sentimeta 81 kwa jike na sentimeta 94 kwa beberu.
Kama ilivyo kwa jamii zote za mbuzi
wa maziwa, mbuzi hawa wanapaswa kuondolewa pembe kwa kuzikata mara kwa mara
tangu wanapokuwa na wiki mbili bada ya kuzaliwa. Hiyo inaleta usalama kwa ajili
ya utunzaji na ukamuaji, hasa ikizingatiwa pia kwamba jamii hii ni wakorofi.
Asili yao
Kama nilivyoeleza hapo awali, Anglo-Nubia
ni mbuzi chotara wa uzao uliopatikana nchini Uingereza baada ya kupandisha jike
la mbuzi wa maziwa wa asili Old English Milch Goat na beberu la Zariby kutoka
India na Russia pamoja na beberu la Nubia kutoka Sudan. Mbuzi hao wamsambazwa
sehemu mbalimbali duniani kwa sasa na huko Marekani wanafahamika kama Nubia tu.
Kwa hiyo, mbuzi wa
Anglo-Nubia halisi ni lazima awe yule ambaye ni mkubwa na mwenye asili
mchanganyiko ya Asia, Afrika na Ulaya ambaye anafahamika kwa utoaji wa maziwa
yenye siagi nyingi.
Kama unataka kuwafuga, wasiliana na ofisa mifugo aliye jirani
ili akuelekeze wapi pa kuwapata pamoja na mambo ya msingi kuyazingatia katika
ufugaji.
Ikiwa una maoni au ushauri, usisite
kunipigia au kunitumia ujumbe wa simu au whatsapp kupitia namba 0656 331974 au
nitumie barua-pepe: maendeleovijijini@gmail.com.
Comments
Post a Comment