Featured Post

MWAMKO WA WANANCHI KUPIMA AFYA ZAO WAONGEZEKA JIJINI MWANZA.

Mkurugenzi wa Shirika hilo, Mugisha Rutasitara, akitoa ufafanuzi juu ya zoezi la Upimaji wa Afya bure pamoja na uchangiaji wa damu kwa hiari, linalofanyika katika uwanja wa shule ya Msingi Mirongo Jijini Mwanza, kuanzia leo hadi jumamosi Julai 16,2016.
Na BMG

Bernadino Ivo Medaa, ambae ni Afisa Uhamasishaji Mpango wa Taifa wa damu salama Kanda ya Ziwa, akitoa ufafanuzi juu ya namna zoezo la uchangiaji wa damu kwa hiari linavyoendelea Kanda ya Ziwa.
Mmoja wa wakazi wa Jiji la Mwanza waliojitokeza kupima afya pamoja na kuchangia damu katika zoezi linalofanyika uwanja wa shule ya Msingi Mirongo kuanzia leo hadi jumamosi.
Mmoja wa wakazi wa Jiji la Mwanza waliojitokeza kupima afya pamoja na kuchangia damu katika zoezi linalofanyika uwanja wa shule ya Msingi Mirongo kuanzia leo hadi jumamosi.
Timu ya Continental Decoder, wauzaji wa Ving'amuzi nchini wakiwa wamejipanga kwa ajili ya kuwahudumia wateja wao. Continental Decoder ni miongoni mwa waliofanikisha zoezi la upimaji wa afya bure pamoja na utoaji wa damu kwa hiari ambalo linafanyika kuanzia leo hadi jumamosi katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mirongo Jijini Mwanza.

Wakazi wa Jiji la Mwanza wamekuwa na mwamko mkubwa wa kupima afya zao hususani kwa magonjwa yasioyopewa kipaumbele ambapo idadi ya watu imeongezeka kutoka 60 kwa kipindi cha mwezi mmoja hadi kufikia 2000 kwa kipindi kama hicho.

Idadi hiyo ni kwa mjibu wa Shirika la Reach and Support All (SARA) la Jijini Mwanza, ambalo linashughulika na masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo afya, elimu pamoja na utatuzi wa migogoro ya kifamilia.

Pamoja na ongezeko la idadi hiyo, Mkurugenzi wa Shirika hilo, Mugisha Rutasitara, ametoa msisitizo zaidi kwa wananchi kuwa na desturi ya kupima afya zao hususani kwa magojwa yasiyopewa kipaumbele ikiwemo uzito, presha na kisukari ili kuepukana na madhara ya kiafya ikiwemo vifo kabla ya wakati.

Rutasitara ameyabainisha hayo hii leo, katika zoezi la upimaji wa afya bure kwa wakazi wa Jiji la Mwanza ambapo ameongeza kwamba wananchi wengi wana tabia ya kwenda hospitalini baada ya kuzidiwa magonjwa, jambo ambalo husababisha uwezekano mdogo wa wao kupona kutokana na kuchelewa matibabu na kwamba jitihana za shirika hilo ni kuhakikisha watanzania wote wanakuwa na desturi ya kupima afya zao mara kwa mara ili kutambua afya zao mapema.

Zoezi la upimaji wa afya bure kwa wakazi wa Jiji la Mwanza, limeenda sambamba na wananchi kuchangia damu kwa hiari ambapo, Bernadino Ivo Medaa, ambae ni Afisa Uhamasishaji Mpango wa Taifa wa damu salama Kanda ya Ziwa, amesema bado kuna changamoto kwa mwananchi mmoja mmoja kuchangia damu ikilinganishwa na wale wanaokuwa katika taasisi za elimu pamoja na dini.

Baadhi ya wananchi waliojitokeza kuchangia damu Jijini Mwanza, wamewatoa hofu wale ambao hawana desturi hiyo kwani hakuna madhara yoyote ya kiafya kwa mtu anaechangia damu huku pia wakiwakumbusha kuwa na desturi ya kupima afya zao mara kwa mara.

Zoezi la upimaji wa afya bure na uchangiaji wa damu kwa hiari Jijini Mwanza, linanyika kwa siku tatu kuanzia leo ambapo Mashirika mbalimbali ikiwemo The Dest and Chair Foundation, Continental Decoder, Mpango Taifa wa damu salama Kanda ya Ziwa pamoja na Reach And Support All, yamesaidia kufanikisha zoezi hilo.

Comments