Featured Post

MKUU WA MKOA WA MBEYA ATEMBELEA PANDAHILL PATAKAPOCHIMBWA MADINI ADIMU DUNIANI YA NIOBIUM KABLA YA KUANZA UCHIMBAJI

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla mwenye suti ya kaki akitembezwa na mwenyeji wake Mkurugenzi wa kampuni ya Pandahil limited ndg Derick ambayo ndiyo inahusika na uchimbaji wa madini ya  adimu aina ya Niobium ambayo hutumika kutengeneza Ndege na computer katika eneo la Songwe Gerezani Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya .(Picha E.madafa, D.Nyembe)
Mkurugenzi wa kampuni ya Pandahil limited ndg Derick ambayo ndiyo inahusika na uchimbaji wa madini ya  adimu aina ya Niobium ambayo hutumika kutengeneza Ndege na computer katika eneo la Songwe Gerezani Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla aneo ambalo litachimbwa madini hayo.

Ramani ya mradi
Na Mwandishi wetu, Mbeya
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla  ametembelea eneo la Pandahill kata ya Songwe mahali ambapo patachimbwa madini adimu aina ya Niobium ambayo hutumika kutengeneza ndege na computer.
 Mpaka sasa madini hayo huchimbwa bara la Amerika tu na kugundulika kwa madini hayo Tanzania utakuwa mgodi wa nne duniani na wa kwanza Afrika
Mkurugenzi wa kampuni ya Pandahil Limited Derick amesema imewachukua zaidi ya miaka 5 kufanya utafiti na kugundua uwepo wa madini hayo, taratibu zote za kisheria zimekamilika na kampuni hiyo itawekeza zaidi ya shilingi bilioni 500 katika mradi huo na mradi utatengeneza ajira watu 500 na mradi huo utaanza uzalishaji mapema mwaka 2018.
Mkuu wa mkoa ameipongeza kampuni hiyo kwa ugunduzi na uwekezaji huo mkubwa sanjali na kuwataka na kutoa ushirikiano na ushirikishwaji wa kwa viongozi na wananchi kwa kila hatua ili kuweka wazi mradi huo kwa wananchi.
Aidha amewataka wananchi na viongozi kutoa ushirikiano kwa kampuni hiyo ili wananchi wanaozunguka eneo hilo uzalishaji utakapoanza wafaidike na ajira, huduma za jamii na kodi mbalimbali kwa hslmashauri na serikali kuu
 Pia amewashukuru kwa mchango wa madawati 400 ambayo yatasambazwa kwa shule 7 zilizokuwa na upungufu wa madawati
 Hata hivyo Gereza la Songwe mkoani Mbeya linatalaji kuvunjwa na kuhamishiwa sehemu nyingine kupisha uchimbaji wa madini hayo adhimu ya duniani ya  niobium baada ya madini hayo kugundulika kuwepo karibu na maeneo ya gereza hilo la songwe.
 Kwa mujibu wa taarifa za wataalam zinadai kuwa madini ya mgodi huo huchanganywa na metali zingine na vyuma vyake hutumika kwenye ujenzi bomba la kupitishia mafuta sanjali na metali zake kutumika katika injini za ndege ili kuzuia mitambo yake kutopata joto kali.

Comments