Hili ni beberu la mbuzi jamii ya Oberhasli
Jike la Oberhasli
Majike wa Oberhasli
Zamani wakijulikana zaidi kama
Swiss Alpine kutokana na
asilia yao kuwa kwenye Milima ya Alps hasa katika wilaya ya Oberhasli katika
eneo la Bernese Oberland katikati ya Uswisi, mbuzi hawa wanafahamika kutokana
na tabia ya upole. Rangi ya ngozi ni udongo mwekundu lakini wana mabaka meusi,
ingawa baadhi ya majike ni weusi kabisa.
Mbuzi jike mkubwa ana uzito wa
kilogramu 54 wakati beberu ana uzito wa kilogramu 68. Kimo cha jike ni
sentimeta 71 wakati dume ni sentimeta 76.
Jike wa Oberhasli anaweza kuzalisha
wastani wa lita 726 kwa mwaka za maziwa yenye wastani wa asilimia 3.6 ya mafuta.
Kama unataka kuwafuga mbuzi hawa, ni
vyema ukamtafuta ofisa mifugo aliye jirani nawe ili akuelekeze namna ya
kuwapata.
Comments
Post a Comment