- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Beberu la Saanen
Jike la Saanen
Na Daniel Mbega
Mbuzi jamii ya Saanen ni wakubwa
na ndio watulivu zaidi kati ya jamii za
mbuzi wa maziwa. Saanen ama Holstein ni mbuzi wazuri zaidi kwa maziwa ambao
wanatoa maziwa mengi sana ingawa yana mafuta kidogo kulingana na maziwa ya
mbuzi wengine. Wastani wa mafuta ni asilimia 2.5 hadi 3.5.
Mbuzi jike wa Saanen anaweza kutoa
wastani wa paundi 1,900 za maziwa kwa mwaka. Kwa kawaida jike mkubwa anaweza
kuwa na uzito wa kilogram 65 wakati beberu anaweza kuwa na uzito wa kilogramu
77.
Utawatambua mbuzi hao kutokana na
umbile lao kubwa na tabia ya upole na utulivu, huku ngozi zao zikiwa laini na
rangi ya maziwa na nyeupe. Masikio yao yamesimama kuelekea mbele.
Mbuzi hawa hawapendi sana jua na
wanazalisha maziwa mengi katika mazingira ya baridi. Kama unawafuga kwenye
maeneo ya joto kama Pwani, ni vyema kuwatengenezea vivuli vya kutosha.
Mbuzi hawa ni wapole na wafugaji
wanawapenda kwa tabia hiyo kwa sababu ni wepesi kuwahudumia hata na watoto.
Asili ya mbuzi jamii ya Saanen ni
kwenye Bonde la Saanen kusini mwa Canton Berne, Uswisi. Mwaka 1893 maelfu
kadhaa ya mbuzi hawa walitolewa kwenye bonde hilo na kusambazwa Ulaya. Kati ya mwaka
1904 na miaka ya 1930, takriban mbuzi 150 wa Saanen walisafirishwa kupelekwa
Marekani kutokea Uswisi.
Ikiwa una maoni au ushauri, usisite
kunipigia au kunitumia ujumbe wa simu au whatsapp kupitia namba 0656 331974 au
nitumie barua-pepe: maendeleovijijini@gmail.com.
Comments
Post a Comment