Featured Post

TBL GROUP YALIPA KODI YA SHILINGI BILIONI 81


Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group, Roberto Jarrin (wa pili kulia) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari , wakati lipokuwa akitoa tathmini ya utendaji kazi wa kampuni hiyo kwa kipindi cha mwaka jana na kutangaza mikakati ya  mwaka  huu,mkutano huo ulifanyika  makao makuu  ya kampuni  hiyo Ilala jijini Dar es Salaam Mei 26,2016.


Mwandishi wa gazeti la The East Africa Kidanka Christopher akiuliza swali kwa Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group, Roberto Jarrin  (hayupo pichani) kuhusiana na uzalishaji wa pombe za asili, wakati wa mkutano na wandishi wa habari wa kutoa tathmini ya utendaji kazi wa kampuni hiyo kwa kipindi cha mwaka jana na kutangaza mikakati ya  mwaka  huu,mkutano huo ulifanyika  makao makuu  ya kampuni  hiyo Ilala jijini Dar es Salaam leo Mei 26,2016.

Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali waliohudhuria katika mkutano wa TBL Group , wa kutoa tathmini ya utendaji kazi wa kampuni hiyo kwa kipindi cha mwaka jana na kutangaza mikakati ya  mwaka  huu, wakimsikiza kwa makini, Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group ,Roberto Jarrin (hayupo pichni) wakati wa mkutano huo ulifanyika  makao makuu  ya kampuni  hiyo Ilala jijini Dar es Salaam,  leo  Mei 26 2016.
Meneja wa afya na Usalama wa TBL Group Renatus Nyanda akitoa maelekezo kwa waandishi wa habari  juu ya utembeaji ndani ya kiwanda cha Tbl Ilala jijini Dar es Salaam.ambapo waandishi w habari walipata fursa ya kutembelea maeneo mablimbali ya uzalishaji wa bia kiwndani hicho leo Mei 26,2016.

Baadhi ya wandishi wa habari wakitembelea maeneo ya uzalishji w kiwanda cha TBL Ilala jijini Dar es Salaam.

Waandishi wa habari kutoka vyombo mablimbali wakipata maelezo ya uzalishaji wa bia kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa TBL Group leo Mei 26,2016 wakati walipotembelea kiwanda hicho.
Mtalamu wa upishi wa vinywaji wa TBL Group (Techincal Brewer) Emanuel Sawa akiwaonyesha waandishi wa habari moja ya bia aina ya Castle Luger, jinsi ianavyozalishwa wakati wlipotembelea kiwand hicho mara baada y kumalizika kwa mkutano wa  tathmini ya utendaji kazi wa kampuni hiyo kwa kipindi cha mwaka jana na kutangaza mikakati ya  mwaka  huu, ulifanyika  makao makuu  ya kampuni  hiyo Ilala jijini Dar es Salaam leo Mei 26,2016.

Mtaalam Mkuu wa Upishi wa Vinywaji wa TBL Group ,Cavin Inkya, akiwafafanuliaa jambo waandishi wa habari wakati walipotembelea eneo la vinu vya kupikia bia.

Kampuni ya TBL Group imelipa kodi ya mapato ya kiasi cha shilingi bilioni 81 katika kipindi cha mwaka 2015.
Akitoa  taarifa ya tathmini ya utendaji wa kampuni ya mwaka uliopita kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin pia amebainisha kuwa mbali na kampuni kulipa kiasi hicho cha kodi pia imekusanya kodi za serikali kiasi cha shilingi bilioni165 ikiwa ni kodi ya mlaji (exercise duty) ,bilioni 114   ikiwa ni kodi ya ongezeko la thamani (VAT) na bilioni 24 ikiwa ni malipo ya kodi nyinginezo ikiwemo kodi ya PAYE.

TBL Group ni kampuni inayoongoza  kulipa kodi nchini ikiwa imechagia pato la serikali kwa njia ya kodi kiasi cha shilingi Trilioni 2.3 katika kipindi cha miaka 10 “Kampuni yetu imechangia maendeleo ya taifa kwa njia ya kukusanya na kulipa kodi na mchango huo umekuwa ukitambuliwa na taasisi mbalimbali na kuitunukia tuzo ikiwemo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambayo imeitunukia tuzo ya Mlipa kodi bora nchini kwa kipindi cha miaka mine mfululizo”.Alisema Jarrin.
TBL Group inajumuisha  makampuni ya- Tanzania Breweries Limited (TBL), Tanzania Distilleries Limited (TDL)  na  Dar Brew Limited.Biashara kuu ya kampuni ni kuzalisha na kuuza vinywaji ikiwemo bia za aina mbalimbali,vinywaji vikali na vinywaji vya asili..  

Jarrin alibainisha hayo wakati akitoa ripoti ya utendaji wa kampuni katika kipindi cha mwaka 2015 na mikakati yake ya mbele katika kipindi cha mwaka 2016/17 kwa waandishi wa habari “TBL Group itaendelea kuunga jitihada za serikali zakukuza sekta ya viwanda nchini kwa kuendelea kujenga viwanda nchini na tangu kampuni hiyo ibinafsishwe mwaka 1994,imekuwa ikiendelea kuwekeza na tayari imewekeza Zaidi ya shilingi bilioni 150 kwa ajili ya kujenga viwanda vilivyokuwepo awali uwa vya kisasa Zaidi kuendana a teknolojia ya kisasa

Kampuni inavyo viwanda 10 nchini na miongoni wa viwanda vyake vilivyopo katika mikoa ya Mwanza,Mbeya na Dar es Salaam vimetunukiwa tuzo mfululizo za kuwa viwanda bora katika viwanda vinavyomilikiwa a kampuni mama ya SABMiller katika bara la Afrika.TBL Mwanza na Mbeya vikiwa katika kundi la viwanda 10 na 15 kwa ubora duniani.

Jarrin alisema biashara ya bia za kampuni ya TBL zinatawala soko kwa asilimia 78 nchini ikiwa inaongozwa na aina za bia za Safari, Kilimanjaro, Ndovu, Castle lager na Castle Lite .Pia kampuni inatengeneza  mvinyo na vinywaji vikali maarufu vinavyotamba kwenye soko kwa asilimia 73 ambavyo ni   - Konyagi, Valuer and Dodoma Wine -  Kwa upande wa vinywaji vya asili vinywaji vyake vinatawala soko kwa asilimia 8 ambavyo ni – Chibuku and Nzagamba -   Utafiti uliofanywa na taasisi ya CanBack kuhusiana na matumizi ya  pombe za asili nchini umebainisha kuwa matumizi ya pombe za asili nchini ni asilimia 50%

 Jarrin aliendelea kueleza kuwa TBL Group inaendelea kutoa mchango wa kukuza uchumi wa taifa kupitia katika sekta ya uuzaji vinywaji ambayo imetoa ajira zaidi ya milioni 2 za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja zinazoendelea kuwanufaisha watanzania wa kada mbalimbali.Kwa upande wa sekta ya kilimo wakulima wa zao la Shahiri Zaidi ya 3000 wamenufaika kupitia mpango wa kushirikiana na kampuni.Katika kipindi cha mwaka 2015 mpango huu umewezesha ongezeko la uzalishaji wa zao hilo kufikia tani 15,574 kiasi ambacho kimevuka lengo la matumizi na mahitaji ya kampuni.
Pia imebainishwa kuwa zaidi ya wakulima 700 wananufaika na mpango wa kiwanda cha TDL wa kushirikiana nao atika kilimo cha zabibu kinachoendeshwa katika vijiji vya  Bihawana, Mpunguzi,, Mvumi, Hombolo, Mbabala, Veyula, Makang’wa, Mzakwe na Mbalawala .Chini ya mpango huo wakulima wanawezeshwa kupatiwa utaalamu wa kilimo kwa kushirikiana na taasisi yaMakutupora Viticulture Training and Research Center (MVTRC). Pia chini ya mpango huu watoto wa wakulima wa zao la zabibu wamekuwa wakisaidiwa kielimu kupitia  mfuko unaojulikana kama Zabibu na Shule Kwanza.

Jarrin pia alibainisha kuwa kampuni ya DarBrew imeweza kuleta mapinduzi ya uuzaji wa pombe za asili nchini kwa kuwawezesha watumiaji kupata kinywaji cha Chibuku na Nzagamba kikiwa kimefungwa kwa viwango mbalimbali na  katika mazingira ya usafi yanayolinda afya za watumiaji na hivi sasa imekuja na mkakati wa kuwainua akina mama kimapato kupitia kuuza bidhaa zake unaojulikana kama Chibuku Mamas ambao hadi kufikia sasa wanawake wapatao 130 wameishajiunga na mpango huu.

Kuhusu mtazamo wake wa hali ya biashara ya kampuni kwa sasa Jarrin alisema sekta ya uuzaji wa vinywaji inakabiliwa na changamoto mbalimbali mojawapo ni bei kubwa ya bia ambayo watumiaji wake wengi wanashindwa kuimudu,kuwepo na vinywaji visivyo katika mfumo rasmi wa ushindani katika soko,kukosekana kwa motisha katika uzalishaji wa malighafi za kutengeneza vinywaji nchini kwa kuwa zinatozwa kodi kubwa ya zuio kuliko malighafi zinazotolewa nje ya nchi.

Alisema baadhi ya mambo yanayostahili kufanyika katika uboreshaji wa sekta ili iendelee kuchangia pato la taifa ni kupunguza  kodi za malighafi zinazozalishwa nchini kama kimea kinachotumika kutengeneza bia pia kulasimisha pombe za asili  ziende sambamba na vinywaji vya sili vinavyolipiwa kodi na kuhakikisha  vinywaji vya asili vinapatikana katika mazingira ya usafi “Pamoja na changamoto nyingi zilizopo katika sekta hii tunaendelea kukabiliana nazo na tumedhihirisha uwezo wetu kwa kuwa na viwanda vyenye ubora wa hali ya juu nchini Tanzania,” alisema Jarrin.

Comments