Featured Post

RIADHA TANZANIA WAMPONGEZA JAMAL MALINZI

SHIRIKISHO la Riadha Tanzania (RT), linapenda kuwapongeza wajumbe wa mkutano mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kwa kufanikisha uchaguzi kwa amani na kumchagua Jamal Emilio Malinzi kuwa Rais mpya, katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 27 jijini Dar es Salaam.
Rais wa RT, Anthony Mtaka, ametoa salamu hizo za pongezi jana, ambako amemtakia kila la heri Malinzi na Kamati yake ya Utendaji katika majukumu yao ya kusimamia na kuongoza soka la Tanzania.
Mtaka ameelezea imani kubwa aliyonayo kwa Malinzi na timu yake na kuwatakia mafanikio mema katika utendaji.
Pia amebainisha kuwa, RT itatoa ushirikiano kwa TFF pale itakapohitajika kwa maslahi ya maendeleo ya michezo nchini.

Comments