Featured Post

OMARI KIMWERI KUWA MTANZANIA WA KWANZA KUWANIA UBINGWA WA DUNIA WA WBC


BONDIA Omari Kimweri 'Lion Boy' anayefanya shughuli zake Deer Park, Victoria, nchini Australia anatarajia kuwa Mtanzania wa kwanza kupanda ulingoni Novemba 30 kugombea ubingwa wa dunia unaotambuliwa na Baraza la Ndondi la Dunia (WBC) katika uzani wa Kg47.5.
Mpambano huo utapigwa nchini China Novemba 30 na Mchina Xiong Zhao Zhong ambaye ni bingwa wa dunia wa WBC minimum weight anayeshikilia taji hilo kwa sasa katika uzito huo.
Kimweri anakuwa mtanzania wa kwanza kuwania taji kubwa kabisa Duniani akitokea nchini Austalia uku sapoti kubwa akitegemea kutoka Tanzani ambapo alipozaliwa 
na kigezo cha kufanya apate pambano hilo kubwa ni kutokana na rekodi yake pamoja na kutakiwa mtu ambaye anatokea bara la Afrika ambapo kula imemdondokea bondia Omari Kimweri kwa mara ya kwanza mtanzania huyo ataonekana dunia nzima akijaribu kuwania ubingwa wa WBC.
Ambapo ni kiu ya mabondia wengi duniani kumiliki mikanda mikubwa ya kimataifa Kimweri mwenye rekodi  ya kucheza michezo 16 ambapo ameshinda michezo 13 na kuchezea kichapo michezo 3  na mpinzani wake.
Omari Kimweri and Randy Petalcoria

Xiong Zhao Zhong amecheza michezo 26 akishinda 21 kupigwa 4 na kutoka droo mmoja. 
Mabondia hawo wote vijana wenye umri mdogo wa miaka 31 wate wawili wakitofautiana mwezi mmoja tu katika kuzalia mpambano huo umekuwa gumzo katika nchi tatu kwa sasa kwani kila mmoja anajiandaa kivyake.
Kimweri kwa sasa anaefanya mazoezi makari uku akipewa sparng na bondia  Randy petalcoria  wa Philippines ambaye ni bingwa wa  light fly weight.
Omari Kimweri kwa sasa yupo katika mazoezi mazito ya kujiandaa na mpambano huo huku akitegemea zaidi duwa za watanzania kwa kuwa ushindi wake ni ushindi wa Watanzania wote. Mungu Ibariki Tanzania! Mungu Mbariki bondia Omari Kimweri.
CHANZO: superboxingcoach blogspot

Comments