Featured Post

MAJERUHI FLAMINI KUKOSA MECHI MUHIMU ZA ARSENAL

KIUNGO wa Arsenal Mathieu Flamini atakuwa nje kwa wiki mbili hadi tatu kutokana na maumivu ya kende aliyoyapata Jumamosi katika mechi waliyoshinda 2-0 nyumbani kwa Crystal Palace.
Nyota huyo mwenye miaka 29 ataikosa mechi ya leo Jumanne ya Kombe la Ligi dhidi ya Chelsea na mechi ya Jumamosi dhidi ya Liverpool.
Pia anaweza asiwemo kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Borussia Dortmund Novemba 6 na safari ya kuikabili Manchester United siku nne baadaye.
Flamini amekuwa mchezaji muhimu tangu arejee klabuni hapo mwezi Agosti.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa amepongezwa kwa kufanya vizuri tangu alipotua hapo akitokea AC Milan kwa usajili huru huku Arsenal ikiwa haijapoteza hata mechi moja katika zote alizocheza.
Kikosi cha Arsene Wenger kinaongoza Ligi Kuu baada ya mechi tisa lakini mbali ya ushindi a 1-0 dhidi ya Tottenham, hawajakutana na timu yoyote ya Ligi Kuu ambayo msimu uliopita ilikuwa kwenye saba bora, kwahiyo kumkosa Flamini katika wakati huo muhimu kunaweza kukayumbisha timu hiyo kwenye kiungo.
Mikel Arteta, aliyepewa kadi nyekundu katika mechi dhidi ya Crystal Palace, ataikosa mechi dhidi ya Chelsea lakini atakuwepo katika mechi dhidi ya Liverpool.
Arsenal pia wanaongoza kundi lao kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Hata hivyo, wana pointi sawa na Borussia Dortmund, ambayo ilishinda Emirates kwa mabao 2-1 mwezi huu, na Napoli, ambayo wamekwishaifunga. 
CHANZO: BBC

Comments