Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa
Aweso kushoto akionyeshwa na
wananchi wa Kijiji cha Manolo Kata ya Manolo wilayani Lushoto maji
wanayotumia kutoikana na kukabiliana na uhaba wa maji wakati wa ziara
yake juzi iliyokuwa na lengo la kukagua miradi ya maji na kuzungumza na
wananchi.
Naibu
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akizungumza na wananchi wa
Kijiji cha Mgwashi Halmashauri ya Bumbuli wilayani Lushoto wakati wa
ziara yake
Naibu
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akikagua vyanzo vya maji
kwenye Halmashauri ya Bumbuli wilayani Lushoto wakati wa ziara yake
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akikagua
vyanzo vya
maji kwenye Halmashauri ya Bumbuli wilayani Lushoto wakati wa ziara yake
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akipata
maelekezo wakati wa ziara yake ya akikagua vyanzo vya
maji kwenye Halmashauri ya Bumbuli wilayani Lushoto wakati wa ziara
yake katikati ni mhandisi wa maji Halamshauri hiyo Samadu Makau
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akiwa
amebeba ndoo ya
maji kwenye kijiji cha Mgwashi wilayani Lushoto wakati wa ziara yake
NAIBU
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso amewaonya wahandisi wa maji
nchini wanaoshindwa kusimamia miradi ya maji kwenye maeneo yao na
kupelekeea fedha zinazotolewa na serikali kushindwa kutumika kama
iliyokusudiwa badala yake wanazitumia kulipana posho. Kauli ya
Naibu Waziri huyo aliitoa juzi wakati wa ziara yake ya kutembelea
Halmashauri ya Bumbuli wilayani Lushoto alipokuwa akikagua miradi ya
maji huku akilazimika tena kumsimamisha kazi Mhandisi wa Maji Samadu
Makau kutokana na kushindwa kusimamia vema mradi wa Maji Mgwashi wenye
thamani ya zaidi ya Bilioni 1.5 na kupelekea wananchi kukosa maji. Naibu
Waziri ambaye alianza ziara yake mkoani Tanga kwenye wilaya ya
Handeni,Korogwe,Lushoto na Halamshauri zote ndani ya wilaya hizo ambapo
alibaini kuwepo kwa ubadhirifu mkubwa wa fedha za serikali katika miradi
ya maji tokea mwaka 2012 kutokana na kutokuwepo kwa usimamizi makini wa
watendaji wa serikali. Alisema ubadhirifu na upotevu wa fedha
za Serikali inatokana na wahandisi wa maji wa mikoa na wilaya waliopewa
jukumu la kusimamia miradi hiyo na kushauri kushindwa kuwajibika
ipasavyo hivyo kupelekea kuingiza hasara na kupelekea wananchi kukosa
maji hivyo Wizara kuanza kutilia mashaka taaluma zao. Naibu
Waziri huyo alisema haiwezekani serikali inapeleka fedha nyingi kwenye
miradi ili kuweza kutatua tatizo la uhaba wa maji kwa wananchi huku
wahandisi hao wa maji wakishindwa kusimamia kwa waledi miradi hiyo huku
Serikali ikiwalipa fedha za mishahara kwa ajili ya kuisadia majukumu
hayo. “Haiwezekani Serikali inatumia fedha nyingi sana
kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama kwa lengo la
kuondokana na adha hiyo huku wahandisi waliopo kwa niaba ya Serikali
wakishindwa kuisimamia badala yake unapewa taarifa ya ubabaishaji kila
maeneo ya miradi unapotembelea”Alisema. “Kutokana na mradi huu
kutumia muda mrefu bila kuwepo kwa mafanikio yoyote ni dhahiri Mhandisi
utakuwa umeshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo hivyo niagize
asimame kazi hii kwani haweze kutusaidia kwenye masuala ya maji hivyo
ukae pembeni utipishe maana hauna msaada kwetu “Alisema. Kabla
ya kuchukua maamuzi hayo Naibu Waziri Aweso alisema eneo la Mgwashi
kumekuwa na changamoto kubwa kutokana na serikali kupeleka fedha nyingi
lakini maji wananchi hawajaweza kupata huduma ya maji ili kuweza
kuendana na azma ya Rais Dkt John Magufuli ya kumsaidia kumtua ndoo
kichwani mwanamama ikiwemo kutokutembea umbali usiozidi mita 400. “Lakini
hata mbunge wenu hapa January Makamba ameniambia kuhusu mradi huu wa
Mgwashi umekuwa kama una magumashi umetumia fedha nyingi lakini maji
hayaonekani hata yanayopatikana umbali mrefu na kupelekea shida kwa
wananchi kutembea umbali mrefu hii sio sawa kabisa” Naye kwa
upande wake,Mhandisi wa Maji Halamshauri ya Bumbuli,Makau alimueleza
Naibu Waziri huyo kuwa mradi huo ulioanza mwaka 2009 na ulitakiwa uwe na
tanki mmoja la ujazo wa lita 225,000 na matenki mawili ya ukarabati
huku moja ya tanki hilo likiwa na lita 225000 lilopo katika kijiji cha
Kihitu huku tenki lengine 90 elfu tisini. Alisema mradi huo una vituo 54
vya kuchotea maji kutokana na aina iliyofanyika hivyo mateki ya huku
mawili ililoukatabati 225,000 na elfu 90 linatakiwa kuhudumia vituo 45
wakati la huku linatakiwa kuhudumia vituo vyengine vilivyobakia ili
kukamilisha idadi husika.
Comments
Post a Comment