- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma
akihutubia Baraza la Wafanyakazi wa
Mahakama ya Tanzania leo Jijini
Dodoma.
NA BEATRICE LYIMO-MAELEZO, DODOMA
JAJI Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma,
amewataka viongozi mbalimbali wa mahakama wakiwemo Naibu Wasajili, Mahakimu,
Watendaji, Wakuu wa Idara na Vitengo kutenda haki kwa watumishi walio chini
yao.
Jaji Mkuu aliyasema hayo jana mkoani Dodoma
wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa Baraza la Wafanyakazi wa Mahakama
Tanzania.
“Sisi
kama wasimamizi wakuu wa haki nchini tuna wajibu mkuu wa kutenda haki kwa watumishi
kwa vitendo, ni ukweli usiopingika kwamba kimbilio la mtumishi yeyote
aliyefikwa na matatizo ni kwa kiongozi wake katika sehemu yake ya kazi, hivyo
basi kila kiongozi anapaswa kufungua milango kwa watumishi waliopo chini yake,”
alisema Jaji Mkuu.
Jaji
Mkuu ameongeza kuwa, ubora wa viongozi unapimwa kwa namna wanavyosaidia
wafanyakazi walio chini yao, hivyo kuwataka viongozi hao kutokufunga milango yao
kwa watumishi wanaowaongoza.
Aidha,
Jaji Mkuu amebainisha baadhi ya mafanikio ya kushirikisha wafanyakazi kwa lengo
la kukuza motisha na kuleta ufanisi katika maeneo ya kazi na kuongeza tija
katika uzalishaji.
“Umihimu
wa kushirikisha wafanyakazi usilenge tu katika mabaraza haya ya wafanyakazi bali
uwe endelevu ili wafanyakazi wajione ni sehemu ya mabadiliko yanayoonekana”
amebainisha Jaji Mkuu.
Hata
hivyo Jaji Mkuu ametoa rai kwa viongozi hao kufanya kazi kwa upendo, kutoa
taarifa mbalimbali kwa wafanyakazi hali itakayopelekea kupunguza baadhi ya
migogoro katika maeneo ya kazi.
Mkutano
wa Baraza la wafanyakazi wa Mahakama Tanzania umewashirikisha wajumbe kutoka
kanda zote na menejimenti ya Mahakama Tanzania.
Comments
Post a Comment