Featured Post

WAZIRI TIZEBA NA MWIJAGE WATUA KAGERA





Na Mathias Canal-WK, Bukoba-Kagera

Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba (Mb) na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage wamewasili Mkoa Kagera kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia 10 Julai 2018 hadi 13 Julai 2018.

Ziara hiyo imeanza kwa mawaziri hao kupokea taarifa Mkoa huo iliyowasilishwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Mustapher Kijuu kuhusu sekta ya Kilimo na sekta ya viwanda, biashara Uwekezaji.

Katika ziara hiyo kwa pamoja watakutana na wadau wa kahawa, kutembelea Chama cha msingi Kwarukwazi Wilayani Kyerwa, sambamba na kukutana na wadau wa Kahawa na viwanda vinavyokoboa Kahawa Wilayani Karagwe.

Katika siku ya pili ya ziara hiyo mawaziri hao watatembelea na kuongea na uongozi wa viwanda cha Sukari Kagera, kukutana na wadau wa Kahawa na kutembelea Chama cha msingi cha Kyaka Wilayani Misenyi. 

Tarehe 11 Julai 2018 ikiwa ni siku ya tatu ya ziara hiyo mawaziri hao kwa pamoja watakutana na wadau wa Kahawa na kutembelea Chama cha msingi Izigo Wilayani Muleba.

Comments