Featured Post

TFF YABADILI MFUMO WA LIGI KUU



NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imebadili kupitisha mfumo wa Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara juu ya timu za kushuka na kupanda.

Na kuanzia msimu ujao FDL itachezwa katika makundi mawili yenye timu 12 na timu 1 kutoka kila kundi itapanda kwenda Ligi Kuu wakati timu zitakazoshika nafasi ya pili na ya tatu katika makundi yote zitacheza mtoano kwa mechi za nyumbani na ugenini.
Taarifa ya TFF imesema kwamba washindi katika mechi hizo watacheza na timu zilizoshika nafasi ya 17 na 18 katika Ligi Kuu kupata timu mbili zitakazocheza Ligi Kuu, huku timu mbili za nafasi ya 19 na 20 zikishuka daraja.
Timu hizo mbili za Ligi Kuu zilizoshika nafasi ya 17 na 18 kama zitapoteza michezo yao zitashuka Daraja kuungana na zilizoshika nafasi ya 19 na 20 na TFF imesema kwamba inafanya hivyo ili kuongeza ushindani wa Ligi Kuu, FDL na SDL.


Comments