- Get link
- Other Apps
Featured Post
SERIKALI KUFUTA TOZO YA USAJILI, KUSHIKILIA NA KUHUWISHA DAWA ZENYE IDADI NDOGO ZA WAGONJWA (ORPHAN MEDICINE) KWA WAWEKEZAJI WOTE
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- Other Apps
NA WAMJW-MWANZA
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto imefuta tozo ya usajili, kushikilia na kuhuwisha dawa
zenye IDADI ndogo ya wagonjwa kwa wawekezaji wote kupitia Mamlaka ya Chakula na
Dawa (TFDA).
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati alipotembelea kuangalia ujenzi wa
jengo la TFDA ambalo linajengwa Jijini Mwanza ili kusogeza huduma kwa wananchi
wa mkoa huo.
“Ili kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. John Pombe Magufuli za
kukuza nchi kupitia uchumi wa viwanda hivyo TFDA msiwe kikwazo kwa wawekezaji
hao hivyo kuanzia leo nafuta tozo za kusajili, kushikilia na kuhuwisha dawa
(orphan medicines) ambazo zina idadi ndogo ya wagonjwa na magonjwa hayo ni
hatarishi ili kuvutia wawekezaji katika eneo hili,” alisema Waziri Ummy.
Aidha, Waziri Ummy amewaagiza TFDA kuzipa kipaumbele dawa
hizo wakati wa usajili.
Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa kuendana na juhudi hizo pia
Serikali imefuta tozo ya udhibiti ya thamani ya 0.25 za dawa, vifaa na vifaa
tiba zinazoingizwa kwenye hospitali za Umma kutoka kwa wafadhili.
Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa TFDA ina wajibu wa
kusimamia Tanzania isiwe jalala la bidhaa zisizo na ubora kwa watanzania hivyo
wanatakiwa kuweka afya ya wananchi mbele kuliko manufaa binafsi.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Bi. Agness
Kijo amesema kuwa ujenzi wa jengo hilo ukikamilika utasaidia kuhudumia huduma
za kimaabara kwa bidhaa zinazoingia nchini kwani itakuwa sio lazima tena kwenda
kupima bidhaa hizo jijini Dar es salaam.
“Maabara hizi zikikamilika zitasaidia kufanya vipimo na
udhibiti wa bidhaa katika mipaka mingi ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Silali, Rusumo
na Mtukula ili kuweka usalama wa bidhaa zinazoingia na kutoka nje ya nchi kwa
usalama wa wananchi.
Sambamba na hilo Waziri Ummy alipata nafasi ya kutembelea
kukagua ujenzi wa jengo la wodi ya mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya
Mkoa wa Mwanza Sekou toure na kuhakikisha ujenzi unakamilisha ili kuokoa vifo
vya mama na mtoto vinavyotokana na uzazi.
“Kama watu wa mwanza wanaridhishwa na huduma zinazotolewa
katika hospitali hii basi ni lazima huduma za afya ziboreshwe ikiwemo afya ya
mama na mtoto hivyo ninaleta mashine ya CT Scan kwa ajili ya kuboresha matibabu
hapa,” alisema Waziri Ummy.
Aidha, Waziri Ummy aliwataka watendaji wa Hospitali kutoa
taarifa za utendaji kwa Waziri wa Afya na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo pamoja na
kusimamiwa na Wakuu wa Mikoa yao ili kuimarisha huduma za afya nchini.
Comments
Post a Comment