Featured Post

VIDEO: MAKAMU MWENYEKITI NCCR MAGEUZI AREJEA CCM, AZOA NA WENGINE WATANO



Makamu Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Tanzania Bara, Leticia Mosore, jana Ijumaa alitangaza kurejea CCM baada ya kukunwa na utendaji kazi wa Rais Magufuli.
Mosore alisema kwamba, aliondoka CCM kwa kuwa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi haukuwa wa kuridhisha, lakini sasa anaona mabadiliko makubwa
ambayo yanazidi kuisongesha mbele Tanzania.

Mosore, ambaye aliambatana na wananachama wengine watano wa NCCR-Mageuzi waliorejea CCM, alisema kwamba sababu kubwa ni rushwa na ukosefu
wa maadili, akidai kwamba zilikuwa hoja kuu za upinzani lakini kwa sasa zinatekelezwa ipasavyo na Serikali ya Awamu ya Tano.
"Kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais John Magufuli ameshughulikia kweli kweli rushwa na maadili. Serikali inafanya kazi kwa uwazi, ukusanyaji wa mapato ni mzuri. Pia imedhibiti matumizi yasiyo ya lazima," amesema.
Wanachama wengine wa NCCR-Mageuzi waliojiunga na CCM ni aliyekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya NCCR, Mchata Mchata, aliyekuwa Katibu Jimbo la Segerea, Lilian Kitunga, aliyekuwa Katibu wa Wanawake Segerea, Nossy Chacha, pamoja na Vedalin Nicholaus na Eunice Zacharia.

Comments