Featured Post

'MAJANGILI WA FARU' AFRIKA KUSINI WATAFUNWA NA SIMBA



JOHANNESBURG, AFRIKA KUSINI
Takriban majangili wawili wa vifaru wame raruliwa na kuliwa na simba katika mbuga ya wanyama huko Afrika ya kusini, maafisa wamesema.
Askari wa doria waligundua mabaki ya watu wawili, na wengine wanahisi ni mabaki ya watu wa tatu, katika mbuga ya wanyama ya Sibuya karibu na Kusini-Mashariki mji mwa mji wa Kenton.

Bunduki yenye nguvu kubwa na shoka pia vilikutwa hapo.
Katika miaka ya hivi karibuni, Ujangili umeongezeka sana Afrika ya Kusini, ili kutokana na kuongezeka kwa hitaji la pembe za vifaru huko bara la Asia.
Kwa upande wa China, Vietnum na sehemu nyingine nyingi pembe za vifaru zinaaminika kuwa na sifa ya kuongeza hisia za mapenzi.
Mmiliki wa Hifadhi wa Sibuya, Nick Fox katika taarifa yake kwenye ukurasa wa Facebook wa mbuga hiyo amesema watu hao wanao sadikiwa kuwa ni majangiri waliingia katika mbuga hiyo jumapili usiku au mapema siku ya Jumatatu asubuhi.
"Walikosea na kuingia kwenye eneo la kujidai la simba, ni eneo kubwa hivyo hawakuwa na muda mwingi, " Bwana Fox aliliambia Shirika la habari la AFP.
"Hatuna hakika ni watu wangapi walikuwa - kwani kuna mabaki kidogo sana ya miili yao. "
Mabaki hayo ya likutwa majira ya saa 16:30 siku ya Jumanne.
Timu ya kupambana na ujangili iliwasili katika eneo la tukio, sehemu ambapo bunduki ya uwindaji yenye kifaa cha kuzuia sauti, shoka refu na waya - vifaa ambavyo hutumiwa na majangili vilipatikana.
Ili kupatikana kwa mabaki ya watu hao, ilibidi simba kadhaa kuchomwa dawa za usingizi, bwana Fox aliongeza.
Hata hivyo, Polisi wanaendelea na kupiga doria katika eneo hilo ili kuangalia kama kuna majangili walio nusurika ku uawa na simba hao.
Kwa mwaka huu pekee, Vifaru tisa waliuawa na majangili mashariki mwa jimbo la Rasi, sehemu ambayo hifadhi hiyo ipo.
Hata hivyo, zaidi ya faru 7,000 wameuawa nchini Afrika Kusini katika muongo uliopita pekee.
BBC/SWAHILI

Comments