Featured Post

HATARI: HUU UGONJWA WA ZINAA USIOSIKIA DAWA



UGONJWA usiojulikana sana wa zinaa unaibuka kuwa usiosikia dawa ikiwa watu hawatakuwa waangalifu, wataalamu wameonya.
Ugonjwa huo unaojulikana kama Mycoplasma genitalium (MG) hauna dalili lakini unaweza kuwa na madhara ikiwemo kusababisha utasa kwa wanawake.
MG unaweza kukoswa kutambuliwa na kama hautatibiwa vizuri unaweza kuwa sugu kwa madawa.

Shirika la Uingereza linalohusika na afya ya ngono na HIV limeznzisha shuguhli ya kutoa ushauri.
Nakala yake inalaeza jinsi ya kutambua na kutibu ugonjwa wa MG.
MG ni ugonjwa gani? Mycoplasma genitalium ni bakteria ambayo inaweza inaweza kuambukiza wanaume na kuathiri uume kusababisha vigumu kupitisha mkojo.
Kwa wanawake inaweza kuathiri sehemu za uzazi na kusababisha uchungu na hata kuvuja damu.
Ugonjwa huu unaweza kuambukizwa kwa njia ngono isiyo na kinga kutoka kwa mtu ambaye tayari ana ugonjwa huo, Mpira wa kondomu unaweza kuzuia maambukizi.
Mara ya kwanza ugonjwa huu ulitambuliwa nchini Uingereza mwaka 1980 na unaaminika kuwaathiri asilimia moja au mbili ya watu wote.
MG mara nyingi hauna dalili na hautaji wakati wote matibabu lakini unaweza kukosa kutambuliwa au kuchukuliwa kuwa ugonjwa tofauti.

"Matumizi wa kondomu"
Kuangamziwa ugonjwa wa MG kwa kutumia aina moja ya dawa inayofahamika kama macrolides, kumeshuka kote dunaini. Usugu wa ugonjwa huu unakadiriwa kufikia asilimia 40 nchini Uingereza.
Hata hivyo dawa moja inayojulikana kama azithromycin bado inautibu mara nyingi.
Dkt. Peter Greenhouse, mshauri wa masuala ya ngono huko Bristol anawashauri watu kuchukua tahadhari.
"Ni wakatai ambapo watu wanafahamu kuhusu Mycoplasma genitalium," alisema.
"Kuna sababu nzuri ya kubeba kondomu wakati wa likizo za msimu wa joto na kuzitumia."

Comments