Featured Post

BARABARA YA LAMI YAYEYUSHWA NA JUA KALI



QUEENSLAND, AUSTRALIA
WENYE magari katika eneo moja nchini Australia wamelazimika kuyaacha magari yao baada ya lami kuanza kuyeyuka barabarani.
Tairi za magari ziliharibiwa vibaya na lami na sasa madereva takriban 50 wanadai fidia.

Kisa hicho kilitokea katika jimbo la Queensland siku ya Jumanne.
"Sijawahi kuliona jambo kama hili maishani na taarifa zilipoaza kutolewa jana, lilikuwa jambo la kushangaza sana," meya wa eneo hilo Joe Paronella ameambia ABC.
Maafisa wanasema kisa hicho kilisababishwa na jua kali, pamoja na hali kwamba ukarabati ulikuwa umefanyika wiki iliyopita.
Mkazi mmoja wa eneo hilo Deborah Stacey anasema tairi za magari zilijawa na lami.
Jua kali lilikuwa limewaka baada ya siku kadha za mvua.
"Tulishuhudia wiki ya vioo vya magari kuharibiwa na mvua ... kisha jua lilipochomoza, tunashuhudia haya sasa," ameambia jarida la Courier Mail.
Barabara hiyo inapatikana katika eneo la Atherton Tablelands kusini mwa mji wa Cairns na ilifungwa kwa muda.
Wizara ya uchukuzi ya jimbo la Queeensland imeahidi kwamba watu ambao magari yao yaliharibika watalipwa fidia.

Barabara huyeyuka wakati gani (Uingereza)?
•Lami kwenye barabara nyingi huweza kuyeyuka kiwango cha joto kikifikia 50C
•Takriban 5% ya barabara 80C
•Barabara za lami hushika joto sana na hivyo kiwango chake cha joto kinaweza kufikia 50C jua kali likiwaka.


Comments