Featured Post

WASOMALI KUZICHEZESHA YANGA, GOR MAHIA KOMBE LA SHIRIKISHO



NA MWANDISHI WETU
SHIRIKISHO la Soka Africa (CAF) limetaja waamuzi kutoka Somalia ambao ndio watachezesha mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya makundi kati ya Gor Mahia ya Kenya na Yanga utakaochezwa Uwanja wa Moi Kasarani, Nairobi Julai 18, 2018.

Kwenye mchezo huo, Mwamuzi wa katikati atakuwa Hassan Mohamed Hagi akisaidiwa na Hamza Hagi Abdi, Suleiman Bashir Sh.Abdi na Mwamuzi wa akiba atakuwa Nur Muhidin Mohamed.
Taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesema kuwab, Mtathmini waamuzi atakuwa Jan Olivier Mbera kutoka Gabon na Kamishna wa mchezo ni Simphiwe Brian Xaba kutoka Afrika Kusini atakayeongozana na na mratibu wa mchezo huo, Nomsa Jacobeth Mahlangu.
Aidha, mchezo wa marudiano kwa timu hizo utakaochezwa Julai 29, 2018 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wenyewe utachezeshwa na waamuzi kutoka Mauritius.
Mwamuzi wa katikati atakuwa Ahmed Imtehaz Heeralall akisaidiwa na Cauvelet Louis Ralph Fabian na Akhtar Nawaz Rossaye, na Mwamuzi wa akiba atakuwa Ganesh Chutooree.
Kamishna wa mchezo atakuwa Patrick Kangwa kutoka Zambia, Mtathmini waamuzi ni Louzaye Rene Daniel kutoka Congo wakati Mratibu atakuwa Nasiru Sarkintudu Jibril kutoka Nigeria.


Comments