Featured Post

WANANCHI WAIPONGEZA SERIKALI KWA UPANUZI WA BANDARI



NA JANE MWAKYOMA, RUKWA
Wananchi wa mwambao wa ziwa Tanganyika wameishukuru serikali kwa kutenga fedha bilioni 3 kwa ajili ya upanuzi wa Bandari ya Kasanga ili kukuza pato la taifa.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baada ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), Deus Kakoko, kufanya ziara katika vijiji vinavyozunguka Ziwa Tanganyika wilayani Kalambo, walisema uongozi wa awamu ya tano umekuwa ukisikiliza kilio cha wananchi wa hali ya chini ususani wananchi wa mwambao mwa Ziwa Tanganyika ambapo serikali imeona umuhimu wa kupanua Bandari ya Kasanga  ambayo imekuwa ni muhimu sana kwa wakazi wa mkoa wa Rukwa na imekuwa ikiingizia serikali mapato kutokana na biashara zinazofanyika bandarini hapo.
Walizitaja furusa zitakazowanufaisha wakazi hao wakati wa mladi kuanza na mara baada ya mladi kumalizika ambapo walizitaja furusa hizo wakati wa ujenzi kuanza ambapo wananchi hao walisema watapa ajira wakati wa ujenzi wa bandari hiyo,na biashara itakua ikiwa ni pamoja na kukua kwa kipato cha  mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla ambapo biashara hiyo itaambatana na uvuvi wa kisasa kutokana na upanuzi wa bandari hiyo.
Walisema upanuzi huo utasaidia kuongezeka kwa meli za kisasa kubwa ambapo meli hizo zitasaidia mwingiliano wa biashara na kupanuka kwa biashara zitakazokuwa zikifanyika bandarini hapo ambapo ziwa Tanganyika linapakana na nchi kama Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo na nchi ya Zambia ambao ni wafanyabiashara wakubwa wanaotumia Bandari ya Kasanga kutokana na ushirikiano ambao unafanywa na nchi hizo wa kubadilishana biashara bandarini hapo.
Mkurugenzi wa TPA, Deus Kakoko, alisema ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami umemalizika ambapo alisema kilichobaki ni kutafuta mkandarasi ambaye atajenga bandari hiyo ambapo bandari hiyo imekuwa finyu kutokana na kupanuka kwa biashara ambapo serikali imeona umuhimu wa kujenga bandari ambapo bandari hiyo itakuwa kubwa na yakisasa ili kuongeza kasi na mwingiliano wa biashara bandarini hapo.
Alisema wananchi wa mwambao mwa ziwa Tanganyika ni wakati wao kuchangamkia furusa zitakazotokana na ujenzi wa Bandari ya Kasanga ambapo wakazi watapata ajira,na biashara kupanuka ambapo hoteli za kisasa zitajenga na wakazi watapata ajila kutokana  na huduma zitakazobareshwa katika eneo hilo na biashara nyingi zitakuwa na kukuza pato la taifa nchini.
Alisema pamoja na upanuzi wa Bandari ya Kasanga pia kutakuwepo na biashara haramu ambapo aliziagiza mamlaka husika kuwa makini na mizigo itakayokuwa inaingia bandarini hapo ili kuepusha nchi yetu kuwa na biashara ambayo si harali na inaweza kuleta madhara kwa jamii,
"Tunatarajia meli kubwa zitakuwa zinaleta mizigo na kusafirisha mizigo, sasa kuna boti tutafurahia upanuzi wa bandari lakini tuangalie na kuchunguza mizigo inayotoka na kuingia, mtu anaweza kutumia boti kusafirisha biashara ambayo si harali na mwisho wa siku biashara hiyo unaikuta mitaani, naagiza kila mtu afanye kazi yake usiku na mchana," alisema Deus Kakoko.

Comments